JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Bajeti ya kodi za bia, soda haitufikishi popote

WIKI iliyopita Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa alitangaza bajeti ya mwaka 2012/2013. Nafahamu kuwa mpendwa msomaji umeishasoma mengi kuhusiana na bajeti hii. Kwa mantiki hiyo mimi sitajielekeza katika kuchambua nini kimeongezwa kodi au kupunguzizwa kodi kama ulivyo utamaduni wa makala nyingi.

Tunafahamu sote sasa kuwa bajeti hii ya shilingi trilioni 15 na ushehi hivi, imekuwa ya ujumla mno. Bajeti hii sikuiona kama inalenga kutatua tatizo la njaa, umeme, barabara mbovu, reli, viwanja vya ndege, elimu, afya au hata mahusiano ya jamii. Kiwango kilichotengwa nadiriki kukiita umwagiliaji wa matone (drip irrigation).

Hata Waziri Mgimwa aliyeisoma bajeti hii kwa mara ya kwanza maishani mwake, naamini hadi leo yupo kwenye mshangao. Hajasikia mshindo. Hakuna jipya lililotokana na tangazo lake la bajeti. Labda hizo Sh milioni 50 anazotarajia kupata kutokana na matajiri wenye kuweka majina yao kwenye magari binafsi. Kwa bahati mbaya ingetokea mimi ndiye Waziri wa Fedha, nchi hii ningeishitua mbavu.

Wabunge waibane Serikali bila woga

Wabunge jana walianza kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013. Kama ilivyotarajiwa, mjadala wa bajeti ya mwaka huu wa fedha ni mkali.Wiki iliyopita wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliitwa katika Kamati yao ambayo Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Juhudi za Lowassa kuihangaikia elimu zinapaswa kuungwa mkono

 

Naweza kumpenda au kumchukia sana Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, lakini hata iweje sitajizuia kumuunga mkono mtu yeyote akifanya jambo jema au lenye tija kwa taifa.

 

Siku chache zilizopita, Lowassa aliongoza harambee iliyokusanya Sh. milioni 530 kutoka kwa wadau wa maendeleo ya elimu – fedha ambazo Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye mwenyewe ni mwanachama wake, kilichangia Sh. milioni 20.

 

Ikulu kukarabatiwa kwa Sh bilioni 6

Wabunge kadhaa wamejiandaa kuhoji matumizi ya Sh bilioni 6 zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu. Kiasi hicho cha fedha kimetengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013. Wabunge wanahoji kiasi hicho kikubwa hasa kutokana na kuonekana kuwa kila…

RUSHWA BUNGENI

*Halmashauri Dar zawahonga mil. 25/-
*Mbunge CCM asema Chadema ‘inawaovateki’
Kamati ya Kudumu y Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa inatajwa kuwa miongoni mwa kamati zinazonuka rushwa, na kuna habari kwamba wabunge wengine watatu wataunganishwa na mwenzao katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa.

Ije Jubilee nyingine ya malkia tushibe

Si mapumziko hata kidogo, maana ni sikukuu lakini waliofanya kazi wametoka na vinono. Wengi wataendelea kumwombea Mtukufu Malkia Elizabeth II adumu na serikali iendelee kuridhia maadhimisho ya sherehe zake.