JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Mabavu hayatanzuia mgomo wa madakatri

 

 

 

Kwa wiki nzima sasa nchi yetu imekumbwa na mgogoro mkubwa unaohusisha madaktari na serikali kwa upande mwingine.

Balotelli aichanganya Italia

…Ageuka pia kuwa shujaa barani Afrika

Mapema mwaka huu, Mario Balotelli aliachwa katika timu ya taifa ya Italia (Azzurri) iliyocheza na Marekani Jumamosi, Februari 29, lakini Alhamisi iliyopita ghafla aliichanganya Italia alipoipeleka kucheza mechi ya fainali za Euro 2012 hapo juzi, Jumapili, dhidi ya Hispania mjini hapa.

Kashfa uporaji ardhi kubwa Pinda ahusishwa

*Mmoja wa washirika ajitoa kuepuka aibu

*Ni Chuo Kikuu cha Iowa cha Marekani

*Yabainika wanaleta teknolojia hatari nchini

[caption id="attachment_124" align="alignleft" width="160"]Waziri Mkuu Mizengo PindaWaziri Mkuu Mizengo Pinda[/caption]Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameendelea kubanwa kuhusu uamuzi wake wa kuwasaidia Wamarekani kujitwalia ekari laki nane za ardhi kwa miaka 99 mkoani Katavi.

Kero ya ombaomba wa London

Kwa asili nachukia kuomba bila sababu na nilijengewa tabia hiyo na wazazi waliotumia vyema nguvu zao kujitegemea na kututegemeza.

Nyalandu anavyomhujumu Kagasheki

*Adaiwa kula njama wawekezaji wasilipe kodi

*Aendesha kikao bila Kagasheki kuwa na taarifa

*Bodi ya TANAPA yakataa mapendekezo yake

Mgogoro ulioripotiwa na Gazeti hili la JAMHURI wiki iliyopita kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheni na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, sasa umechukua sura mpya.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu, ameingia matatani tena baada ya kubainika kuwa anashinikiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) lisianze kutoza ‘concession fee’ katika hoteli za kitalii nchini, JAMHURI limebaini.

Uamuzi huo unaikosesha Serikali mapato yanayofikia Sh bilioni 17 kwa mwaka. Jaribio la kwanza la Nyalandu kufanikisha mpango wake liligonga mwamba kwenye kikao chake na menejimenti ya TANAPA, kilichofanyika Juni 8, mwaka huu mjini Moshi.