Author: Jamhuri
Natabiri Nyalandu atakuwa tatizo
Siku chache baada ya uteuzi wa viongozi wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii – waziri na naibu wake, niliandika waraka mahsusi uliowahusu. Moja ya mambo niliyoyazungumza ni namna wizara hii ilivyo na vishawishi vingi vinavyotokana na ukwasi wake.
Hotuba ya jk
Kuna madai ya madaktari yasiyotekelezeka – Rais Kikwete
Mapema mwezi huu, Rais Jakaya Kikwete alihutubia Taifa kama ilivyo ada ya utaratibu wake aliojiwekea kila mwezi. Pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alizungumzia mgomo wa madaktari ulioathiri huduma za afya katika baadhi ya hospitali za umma nchini. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba hiyo iliyogusia suala la mgomo wa madaktari.
Madaktari Bingwa Dar watoa masharti magumu
Hili ni tamko la madaktari bingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hawa wanahusisha hospitali za umma za Muhimbili (MNH), MOI, Ocean Road na Hospitali za manispaa katika mkoa huo.
CCM iwabaini, iwatimue wanaoihujumu
Jumatano iliyopita, baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kata mbili za Azimio wilayani Temeke na Tandale, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, waliandamana ili kupinga hujuma walizodai zinavuruga uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho na jumuiya zake zote unaoendelea hivi sasa.
Tamko ya Bodi ya Wadhamini MNH
Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika hospitali.
Nidhamu itawapa wabunge heshima
WIKI hii tumeshuhudia michango mbalimbali ikitoka kwa wabunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Yametokea malumbano kati ya wabunge kadhaa na kiti cha Spika. Binafsi nilishuhudia tukio hili, hadi Mwenyekiti wa Bunge aliyekuwa amekalia kati cha Spika akaamuru mbunge mmoja kuondolewa ukumbini. Mabaunsa sita, walikwishajongea kwa nia ya kumtoa ukumbini, lakini yeye akajitoa mwenyewe.