JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Mahakama imekalia haki yangu miaka 16

Mhariri wa JAMHURI nimevutiwa kwa kiwango kikubwa baada ya kusoma toleo lenu Na 39 la Agosti 14-20, 2012 lililoongozwa na habari yenye kichwa kisemacho ‘Majaji Vihiyo Watajwa’. Mara tu niliposoma habari hii, nikaona ni vyema nifunge safari na kuja hapo ofisini kwako nieleze kilio changu. Wengi wa majaji waliotajwa wameshiriki kwa namna moja au nyingine kukandamiza haki yangu.

Bunge la sasa linaelekea wapi? (2)

Duniani kote upinzani huwa una tabia ya kuchokonoa upungufu wa hoja na kisha kuonyesha vipi maboresho yangekuja kama wao wangeongoza Serikali. Hii maana yake bungeni unakuwapo ukosoaji wa aina mbili.

Balozi za Tanzania aibu tupu

 

*Baadhi hawajalipwa mishahara miezi sita, zimeajiri Wakenya

*Ufaransa pango Sh milioni 720, wanatumia anwani ya Uganda

*Ofisi zinaporomoka, Kikwete asema Richmond imeiponza nchi

*Membe alia Serikali kukata bajeti yake ikabaki asilimia 44 tu

 

Sura na heshima ya Tanzania nje ya nchi inashuka kwa kasi kubwa, kutokana na Serikali kuzitelekeza balozi zake nje ya nchi.

Yapo mambo mengi ya aibu yanayowakumba mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi, kwani baadhi ya balozi zinashindwa kulipia huduma ya simu, maji, umeme na baadhi ya magari yanazimika na kuwashwa kwa kusukumwa kama ya uswahilini. Taarifa ya ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea balozi mbalimbali imeibua uozo wa ajabu.

Majaji maji shingoni

*Maelezo ya Jaji Ramadhani, Luanda moto

*Ripoti ya Ikulu nayo yataka waondolewe

*Lissu ataka wapime, kumshitaki Kikwete

*Amtaka Jaji Kiongozi Fakih Jundu ajiuzulu

 

Mhimili wa Mahakama umetikisika baada ya kuwapo ushahidi wa wazi kwamba Rais Jakaya Kikwete amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwa kuwaongezea mikataba ya kazi baadhi ya majaji na kumpandisha cheo mwingine.

Kennedy: Tusiichekee vita

“Mwanadamu anapaswa kumaliza vita, vinginevyo vita itammaliza mwanadamu.”

Haya ni maneno ya Rais wa 35 wa Marekani aliyeuawa mwaka 1963. John F. Kenney alikuwa akiamini kuwa dunia inaweza kuwa salama zaidi kwa kutoendekeza vita.

Hongera Mkapa, Kikwete alijiandalia aibu ya Mahalu

Napata wakati mgumu. Napata shida jinsi ya kuanza makaha haya. Napata shida si kwa sababu nina maslahi binafsi, bali kwa sababu nakumbuka hadithi ya mwanafunzi aliyebeba upodo huku akijifunza kurusha mishale ya sumu. Hakuwa mahiri na hakujua jinsi ya kuvuta upinde. Kwa kicheko kikubwa, aliipaka sumu ncha ya mshale, upinde akauelekeza karibu na tumbo lake, kamba ya kurushia mshale ikatokea mbele yake.