Author: Jamhuri
Msekwa ang’olewa Bodi Ngorongoro
*Orodha ya kwenda Ikulu jina lake lakatwa
*Ukomo wake ni Oktoba 5 mwaka huu
*Kilio cha kina Telele, Sendeka chasikika
Jina la Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Pius Msekwa, halimo katika orodha ya majina ya watu wanaopendekezwa kushika wadhifa huo, JAMHURI imethibitishiwa.
Njooni shambani mtajirike
Miezi kadhaa iliyopita kupitia Redio TBC Taifa, ofisa mmoja wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliulizwa swali hili, “Je, inawezekana watu binafsi kufungua mashamba ya miti na kufanya biashara ya kuuza miti ya mbao?”
CWT: Mkombozi au mnyonya walimu?
*Nusu ya mapato yake yanatumika makao makuu
*Walimu wanaendelea kukamuliwa asilimia mbili
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa, katika Mkutano wa Bunge uliomalizika hivi karibuni alichangia Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuhoji matumizi ya mabilioni ya shilingi yanayofanywa Makao Makuu ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya mbunge huyo.
Tumechagua kujenga taifa la wajinga
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa elimu nchini. Nafuatilia kilio na matangazo yanayotolewa kila pahala, yakielezea wanafunzi zaidi ya 5,000 wanaomaliza elimu ya msingi na kufaulu mtihani wa darasa la saba huku hawajui kusoma na kuandika. Si hilo tu lakini nafuatilia pia kaulimbiu kuwa ‘Ualimu ni wito’.
Kila mmoja analalamika
Sifa mpya ya Watanzania sasa ni kulalamika. Malalamiko yameshamiri katika kaya, mitaa, ofisi, sehemu zote za kazi na kila mahali. Kinachosumbua zaidi ni kuona kuwa hakuna aliye tayari kuondoa malalamiko hayo hata kama mwenye dhima hiyo ni yeye mwenyewe.
Uhuru wa habari na magazeti kwa wote
Gazeti la JAMHURI ni miongoni mwa midomo, macho na masikio ya Watanzania na wadau wengine wa habari. Uhuru wa habari – ambao dunia yote inautangaza na kuuenzi kwa sasa – ni haki ya kila raia na chombo cha habari.