JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Kimwili CCM, rohoni ni Upinzani

Nimemsikia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina hazina ya viongozi kama iliyonayo Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baraza la Kata Kwashemshi tupewe semina

Mimi ni msomaji wa Gazeti Jamhuri. Naishi hapa Kwashemshi wilayani Korogwe. Kinachosikitisha ni kwamba tangu mwaka jana tuteuliwe katika Baraza la Kata hakuna semina yoyote ambayo wajumbe tumepewa.   Sasa inatuwia vigumu kwetu kutafsiri sheria. Hali hii ni kinyume kabisa…

Tuwape moyo viongozi wachapakazi

Mhariri,

 

Wakati umefika kwa Watanzania kuzungumza na kupongeza viongozi wachapakazi wachache tulionao nchini. Hii tabia itafanya viongozi wengine wengi wawaige viongozi wachapakazi.

Nasema hivi kwa sababu mara nyingi Watanzania wamekuwa na tabia ya kulaumu bila kuchambua viongozi wale wanaofanya kazi kwa uadilifu. Siandikii mate ilhali wino upo.

Bongo: Matendo kwanza

“Ni wajibu wa viongozi wa Afrika kuonyesha utashi wao wa kisiasa, kwa ajili ya kuhakikisha taasisi za umajumui wa Kiafrika (pan-African) unakuwa chombo murua na kisiwe chombo cha mijadala isiyo na ukomo.”

Haya ni maneno ya aliyekuwa Rais wa Gabon, Omar Bongo, aliyefariki mwaka 2009 baada ya kuitawala nchi hiyo kwa muda mrefu.

Taifa letu lipo njia panda

*Bunge, wabunge, vyombo vya habari, wananchi tujadili

Ninakumbuka baadhi ya michango ya mjadala juu ya bajeti ya mwaka 2012/2013 na jinsi ilivyokuwa ya kichama zaidi kuliko uhalisia. Wabunge wetu walisahau kabisa kusudi kubwa kati ya yaliyowaweka bungeni, yaani utashi wa nchi, kwa maana ya uwakilishi wa mamilioni ya Watanzania waliowaamini na badala yake kwa kiwango kikubwa wakatekeleza utashi wa sera za vyama vyao na utashi binafsi.

Wachezaji wa kigeni wanazididimiza Tanzania, England soka la kimataifa

 

Tangu ilipofuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini Nigeria mwaka 1980, ikatolewa mapema ikiwa kundi moja na wenyeji, Misri na Ivory Coast, timu ya soka ya taifa ya Tanzania hadi sasa haijaweza kuifikia tena hatua hiyo na hakuna matumaini yoyote kama itafanya hivyo tena.