JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Uhuru wa habari na magazeti kwa wote – 2

Wana-JAMHURI, wiki iliyopita mtakumbuka kwamba nilieleza umuhimu wa vyombo vya habari na haja ya kulinda uhuru wake adimu. Nikagusia kiasi jinsi magazeti yanavyofungiwa, kutishiwa au kupewa adhabu nyingine.

Tujifunze kutokuwa wavivu wa kufikiri

Kati ya viongozi waliowahi kuiongoza nchi yetu na nitakaoendelea kuwaheshimu sana na kuwapenda ni Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Nani anasajili wachezaji kati ya kocha na viongozi?

Siku moja tu baada ya Arsenal kufungua pazia la Ligi Kuu ya England msimu huu kwa kwenda suluhu, kiungo mpya wa timu hiyo, Santi Carzola alimuomba kocha wake, Arsene Wenger kuingia sokoni ili kusaka wachezaji wa kuziba mapengo yaliyoachwa wazi na beki Alexander Song na mshambuliaji Robin Van Persie.

Ukabila dhidi ya Profesa Maji Marefu ni upuuzi

Wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Mrisho Gambo, alishuhudia namna Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (Profesa Maji Marefu), anavyopigwa vita ya kikabila na baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali jimboni humo.

Wamiliki wa daladala na machozi yasiyokauka

Baada ya kununua basi dogo (Hiace) la kwanza na kulisajili daladala, nilikutana na ulimwengu mpya wa changamoto za biashara za magari. Changamoto zilipozidi niliazimu kukutana na walionitangulia kwenye biashara hiyo ili nipate hazina ya ushauri.

Sumatra na porojo za kujikosha

Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) inapendekeza kuwapo kwa kanuni kadhaa zinazolenga kupunguza ajali nchini. Katika mapendekezo hayo, Sumatra wanataka umri wa madereva wa magari ya abiria uwe kati ya miaka 30 hadi 60. Wamejikita kwenye hoja hiyo dhaifu kwa imani kwamba vijana chini ya umri wa miaka 30 ndiyo chanzo kikuu cha ajali za mabasi nchini!