JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Kagasheki afyeka Kamati ya Vitalu

*Awatupa Jaji Ihema, Beno Malisa, Daniel Nsanzugwanko

*Pia wamo Mbunge Mwanjelwa, Kijazi, Profesa Rutashobya

*Chanzo ni tuhuma za rushwa ugawaji vitalu vya uwindaji

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ameifuta kazi Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii. Kamati hiyo, pamoja na mambo mengine, imelalamikiwa mno kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wajumbe wake zaidi ya 10.

Wabunge wengine wahongwa tena

 

* Mfanyabiashara tajiri wa Dar es Salaam ahusika

* Baadhi yao waogopa, wazisalimisha kwa Spika

Mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia amewahonga wabunge kadhaa wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, JAMHURI imethibitishiwa. Habari za uhakika kutoka kwa baadhi ya wabunge na Ofisi ya Spika zinasema kwamba rushwa hiyo ilitolewa kama “asante” kwa wabunge hao baada ya kuzuru moja ya vitegauchumi vya mfanyabiashara huyo kilichopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, wiki kadhaa zilizopita.

Migogoro ya ardhi ni janga

Mhariri,

 

Kila siku migogoro ya ardhi inaripotiwa katika nchi yetu. Kuanzia Dar es Salaam hadi mikoani ni migogoro tu.

Mabaraza ya Kata yamesahaulika

Mhariri

 

Mabaraza ya Kata yameanzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 7/85 lakini halmashauri zinazosimamia mabaraza haya zimeyatelekeza kabisa. Mimi ni Katibu wa Baraza la Kata Kwashemshi. Tangu tuteuliwe mwaka jana hakuna mafunzo yoyote yaliofanyika, kitendo ambacho ni hatari sana. Mabaraza haya yamepunguza sana mlundikano wa kesi katika Mahakama za Mwanzo na Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya. Napenda niishauri Serikali yangu kwamba elimu kwa wajumbe hawa ni muhimu sana, kwani ni sehemu nyingi wajumbe wanalalamika kwamba wametelekezwa. Tatizo hili halipo kwa Baraza la Kata Kwashemshi tu bali mabaraza mengi nchini malalamiko ni haya haya.

Waziri Kagasheki atazame kasoro hii

Mhariri   Kwanza tunampongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kwa jitihada anazozifanya za kusafisha Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake kwa jumla kwa kuondoa uozo uliokuwamo ndani kwa kipindi kirefu.   Wakati jitihanda hizo zikifanyika,…

Mandela: Urafiki na adui yako

“Ikiwa unataka kupata amani na adui yako, unapaswa kufanya kazi na adui yako, kisha anageuka na kuwa mdau wako.” Haya ni maneno ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyemaliza vita ya ubaguzi wa rangi kwa kutumia mfumo…