JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Nani anawashika mkono wajasiriamali?

Mwezi mmoja uliopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Barua ya biashara kwa BRELA”. Brela ni Mamlaka ya Uandikishaji Biashara na Leseni. Baada ya kuitoa gazetini niliituma pia barua hiyo huko Brela kwa njia ya barua pepe.

Tanzania siku si nyingi haitatawalika

Kwa siku za karibuni nchi yetu imegubikwa na mambo mengi ya kuudhi. Taifa linapokuwa na polisi wezi, waporaji na wauaji, usitarajie kwamba litaendelea kuwa salama. Taifa linapokuwa na majaji kama wale tulioambiwa na Mheshimiwa Tundu Lissu, hakika tumekwisha.

TAFAKURI YA HEKIMA

Polisi wangeweza kuepusha mauaji ya Mwangosi

Nianze kwa kutoa salamu za rambirambi na pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina.

Wafadhili wa migogoro Loliondo wajulikana

Suala la mgogoro wa Loliondo limekuwa likitawala katika vyombo vya habari kwa miongo kadhaa sasa. Safari hii kuna kampeni inayoendeshwa kwenye mtandao kwa wiki kadhaa sasa. Chanzo cha mjadala huo ni kwamba Serikali ya Tanzania inataka kuwaondoa wafugaji wa Kimasai ndani ya Loliondo ili kupisha biashara ya uwindaji wa kitalii. Kampeni hiyo inaendeshwa na mtandao wa Avaaz.

Polisi wazingatie mambo haya

Vyombo vya habari vimeandika na kutangaza juu ya matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi na vyombo vingine vya usalama nchini. Wadau mbalimbali wamejitokeza kulaani kifo cha mwandishi Daudi Mwangosi ambacho tunadiriki kusema wazi kwamba kimesababishwa na bomu lililofyatuliwa na mmoja wa polisi.

China yaipatia Zanzibar mabilioni

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi ambako Zanzibar itapatiwa Sh bilioni 14.8.