Author: Jamhuri
Mwalimu wa Mwalimu Nyerere alivyoagwa
*Pinda asema yeye ndiye Mwalimu Mkuu wa Taifa letu
*Afa akidai malipo ya kiinua mgongo, fedha za usafiri
*Serikali yaahidi kuendelea kumtunza mjane wake
Kuwafutia leseni hakutoshi, washitakiwe
Mojawapo ya habari zilizobeba uzito katika gazeti hili ni ile inayohusu uchakachuaji wa mbolea, ambao umekuwa ukichangia kudhoofisha juhudi za wakulima katika kujiondolea umaskini.
Rais Kikwete tuokoe Karagwe, Runyogote anatumaliza
Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete, Salaam. Mei 30, 2012, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, walimwandikia Mkurugenzi Mtendaji barua wakimtaka aitishe kikao maalumu cha Baraza la Madiwani, kujadili tuhuma mbalimbali za ufisadi walizozielekeza kwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Kashunju Runyogote.
Hatima ya taifa la wavivu, watunga sera mezani
Mwaka 1946 nilipangiwa na mkoloni kuwa Afisa Kata mashuhuri iliyojulikana kama Liwale, wakati huo ilikuwa na watu wapatao kama elfu mbili tu na kwa kweli walikuwa wengi kiasi cha kunifanya nigawe maeneo mengine yatawaliwe na vijana wenzangu niliowaamini.
Matajiri wahujumu kilimo nchini
Wakati Tanzania ikipambana kujiondoa katika adha ya njaa kwa kuboresha kilimo nchini kupitia mradi wa Kilimo Kwanza, wafanyabiashara wenye uchu wa utajiri wa haraka wanahujumu kilimo. Matajiri hawa wanapewa fedha za ruzuku kusambaza mbolea, lakini wanafanya kufuru. Kinachotokea, badala ya kuwapelekea wakulima mbolea, wanawapelekea mbolea iliyochanganywa saruji, chumvi na mchanga.
Fedha za rushwa Hanang’ zatisha
Vita ya kuwania nafasi ya NEC kupitia Wilaya ya Hanang’ Mkoa wa Manyara, imechukua sura mpya baada ya mmoja wa wagombea wanaoelezwa kuenguliwa kwenye Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Hanang’ kubuni mbinu mpya za kampeni.