Author: Jamhuri
Rushwa uchaguzi CCM inatisha
Uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaelekea ukingoni. Tayari viongozi wa nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya mashina hadi Taifa wameshapatikana. Tunawapongeza waliochaguliwa. Lakini pongezi zetu za dhati kwa kweli tunazielekeza kwa wale waliochaguliwa bila kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Hapendwi mtu UK, hata awe waziri
Tabia ya Waingereza kuzijua na kuzitetea haki zao, inanipa faraja kubwa sana wana-Jamhuri wenzangu. Watu wakubwa wamejikuta wanaanguka kwa mambo yanayotokana na kushindwa kuheshimu wadogo. Mfano wake ni Mnadhimu Mkuu wa Serikali, Andrew Mitchell, anayetota matatani kwa kuwaita polisi wanaoshika lindo kwenye Ofisi za Waziri Mkuu pale Downing Street kuwa ni “kajamba nani” tu.
Yah: Tujiulize, maendeleo yaondoe utamaduni wetu?
Wanangu, wakati wa ujana wetu kulikuwa na starehe nyingi ambazo leo nyie hamuwezi kuzifanya kwa gharama yoyote ile labda mjigeuze na kuomba kwa Mwenyezi Mungu miaka irudi nyuma na mpate nafasi ya kufaidi kama tulivyofaidi sisi.
Afadhali ya ‘ngangari’ kuliko ‘magwanda’ haya (1)
Si siri kuwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, mambo si shwari. Amani na utulivu wa nchi yetu vimetikisika. Nadiriki kusema hivi kwa sababu, tangu Uchaguzi Mkuu wa kwanza uliofanyika mwaka 1995, amani na utulivu vimekuwa vikiyumba kila kukicha.
TanzaniteOne yachimba, yasafirisha tanzanite bila leseni halali
Kampuni ya TanzaniteOne Ltd inayochimba madini ya tanzanite katika eneo la Mererani mkoani Manyara, inaendelea kuchimba madini hayo licha ya leseni iliyoiruhusu kufanya kazi hiyo kwisha muda wake, JAMHURI imeelezwa. Kampuni hiyo kutoka Afrika Kusini, inamiliki mgodi huo kwa asilimia…
TanzaniteOne yachimba, yasafirisha tanzanite bila leseni halali
Kampuni ya TanzaniteOne Ltd inayochimba madini ya tanzanite katika eneo la Mererani mkoani Manyara, inaendelea kuchimba madini hayo licha ya leseni iliyoiruhusu kufanya kazi hiyo kwisha muda wake, JAMHURI imeelezwa.