JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

‘Dokta Nchia’: Mpishi wa Nyerere

*Asema Mwalimu alipofungwa bao hakula

“Dokta Nchia”, kama Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyopenda kumuita, hakuwa daktari wa binadamu au mifugo. Alikuwa daktari wa mlo.

Simulizi ya mjukuu wa Mwalimu Julius kambarage Nyerere

*Amepata kuswekwa rumande kwa kuendesha trekta

Petro John Nyerere ni mmoja wa wajukuu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Baba yake ni John Guido Nyerere, mtoto wa nne wa Baba wa Taifa. Petro ni mmoja wa wajukuu wachache kati ya wengi walioishi muda mrefu na babu yao pamoja na bibi yao, Mama Maria Nyerere.

Tumuenzi Nyerere kwa kufifisha udini

Oktoba 14, mwaka huu, mwasisi na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ametimiza miaka 13 tangu afariki dunia. Siku ya kuadhimisha kifo chake, tumeusikia ujumbe mzito kutoka serikalini, taasisi mbalimbali na watu binafsi, wote wakiahidi kumuenzi kwa mema yote aliyoyatenda.

Anna Mwansasu: Walitaka kumwekea Nyerere damu ya Wazungu

Miaka 13 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, afariki dunia, waliokuwa wasaidizi wake wa karibu bado wana kumbukumbu ya mambo mazito kuhusiana na ugonjwa uliosababisha kifo chake. Si hilo tu, Serikali nayo imewasusa na wengi wanaishi maisha ya tabu haijapata kutokea. Yafuatayo ni mahojiano kati ya JAMHURI na Anna Mwansasu, aliyekuwa Katibu Muhutasi wa Mwalimu Nyerere…

Rais Nyerere alipokosa maji ya kuoga Kibondo

Mwaka 1964, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Tanganyika, alitembelea shule yetu.  Nilikuwa nasoma Seminari ya Kaengesa Sumbawanga. Bendi ya shule yenye vyombo vyote vya brass band tulimpigia wimbo maarufu uitwao “The Washington Post”.

Madaraka Nyerere azungumza

Juzi, tarehe 14 Oktoba 2012, tumetimiza miaka 13 tangu kufariki Mwalimu Julius Nyerere, kiongozi wa kwanza wa Tanganyika huru, na baadaye Tanzania.