Author: Jamhuri
Kinana umeanza vizuri, uendelee, umalize vizuri
Nilikuwa naelekea kukata tamaa kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitakuwa na viongozi wanaokerwa na umaskini unaoendelea kuwanyima Watanzania wengi maendeleo ya kweli.
JKT ni mtima wa Taifa (3)
Nimejaribu kurejea kirefu maneno ya Mwalimu kuonesha uchungu wake kwa wasomi waliosema miili itakwenda, lakini mioyo yao haitakuwa huko National Service.
Maazimio Mkutano Mkuu: Kitanzi kinachoisubiri CCM
*Imeagiza bei za vifaa vya ujenzi zishushwe nchini
*Tofauti ya kipato yaelezwa ikiachwa hivi italeta vurugu
*Ada shule binafsi zidhibitiwe, utozaji dola ukomeshwe
*Yakiri ajira ni bomu, wizara lazima ziandae ajira mpya
*Ushuru na vijikodi vinavyoumiza wananchi vikomeshwe
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano wake Mkuu wa Nane uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, kilitoa maazimio ambayo kimeyaeleza kuwa ndiyo dira yake ya ushindi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Wadau waaswa kuhusu takwimu sahihi
Sekta za umma, binafsi na wadau wa maendeleo kwa jumla, wameshauriwa kuzingatia matumizi bora kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi na fursa kwa jinsia zote katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Bila flyover barabara hizi kazi bure
Ujenzi wa barabara unaendelea kwa kasi katika Jiji la Dar es Salaam. Lengo ni kuhakikisha kuwa foleni za magari zinapungua na hivyo kuondoa usumbufu na kuokoa mabilioni ya shilingi yanayoteketea kila siku. Tunaipongeza Serikali, na hasa Wizara ya Ujenzi kwa kazi hiyo nzuri ambayo inaonekana jijini humo na sehemu mbalimbali nchini.
Yah: Azimio la Arusha na ajira muhimu
Wanangu, leo ni Jumanne nyingine ambayo kwa uhakika imenifanya nikumbuke mambo mengi sana. Mojawapo ni yale maneno yaliyozungumzwa na Mwenyekiti wa TANU pale Mwanza Oktoba 17, 1967. Alizungumzia utekelezaji wa Azimio la Arusha.