Author: Jamhuri
Yah: Kama ningekuwa waziri wa dawa na matibabu…
Wanangu, poleni na kazi na hongera sana kwa kuvuka mwaka 2012. Nasikia mnapeana “Happy New Year” kila ninakopita na mnashangilia kwa nguvu, sina hakika mnashangilia kwa sababu zipi, lakini nafikiri kuumaliza mwaka siku hizi ni kazi ya ziada kutokana na maradhi na misukosuko mingi ya maisha.
Muungano ndiyo mboni ya Tanzania (4)
Vyama vikubwa Visiwani vilikuwa ARAB ASSOCIATION, INDIAN ASSOCIATION na AFRICAN ASSOCIATION. Na kutokana na vyama hivyo, vikajazaliwa vyama kama SHIRAZI ASSOCIATION na UMMA PARTY.
Mwaka 2013 uboreshe michezo Tanzania
Tangu mwaka 1974 wakati Filbert Bayi alipoweka rekodi mpya ya mita 1,500 duniani, Tanzania haijapata mafanikio mengine makubwa kiasi hicho katika riadha na hata michezo mingineyo.
Mwaka mpya tuchape kazi
Leo ni Mwaka Mpya. Ni mwaka 2013. Tunafahamu Januari hii ni kichomi kwa familia nyingi. Iwe kwa matajiri au masikini, waajiri au waajiriwa ni mwezi wa tabu. Kodi za nyumba zinadai, ada za shule zinadai, wenye magari mengi yanaisha bima na hati za njia na hata wenye kununua viatu na nguo kwa msimu zimekwisha, wanahitaji vipya.
Nawaunga mkono wananchi wa Mtwara
Niliposikia kwamba wananchi wa Mtwara wameandaa maandamano kupinga usafirishaji gesi kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam, sikuamini. Kutoamini kwangu kulitokana na dhana iliyojengeka kwa miaka mingi kwamba wakazi wa mikoa ya kusini si “wakorofi” kama walivyo ndugu zao wa mikoa kama Mara, Kilimanjaro au Arusha.
Hali ya hewa inatupelekesha sasa
Kuna kuendelea, lakini katika majanga ya asili ni nguvu kidogo sana mwanadamu anaweza kumzuia anayeyaleta.