Author: Jamhuri
TPB yatenga mil 6/- kutunza mazingira
Katika juhudi za kuisaidia Serikali kukabili mabadiliko ya tabianchi, Benki ya Posta Tanzania (TPB) imetenga Sh milioni sita kugharamia upandaji miti mkoani Mwanza.
Mongela asikilizwe kuhusu makaburi
Wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, aliibua hoja ya mpango wa taifa wa ardhi ya kuzika wafu.
Waislamu wachinje, sisi tule nguruwe wetu
Wiki iliyopita niliandika makala juu ya usaliti wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kwa yeye kuamua kuulisha umma uongo uliozaa madhara ya hali ya juu kwa wananchi wa Mtwara. Sitarudia nilichokiandika, ila niwashukuru wananchi na hasa wewe msomaji kwa mrejesho.
Nimepokea simu nyingi, ujumbe na barua pepe pengine kuliko wakati wowote tangu tuanzishe gazeti hili. Nawashukuru mno wasomaji kwa kueleza hisia zenu. Sitaweza kufafanua kila mmoja alisema nini, ila niseme karibu asilimia 95 ya waliowasiliana na mimi walinipongeza.
Sitanii, walinipongeza kwa kuamua kumfunga paka kengele. Hawakutarajia iwapo ningethubutu kumwambia Zitto kuwa katika hili hapana. Katika masuala ya nchi, siasa tuziweke kando. Alinichekesha msomaji mmoja aliyeniandikia hivi: “Kaka wengine wanatuchochea tupigane vita maana wanajua mambo yakiharibika kwetu watarudi kwao.”
Usiniulize ni nani mwenye uraia wa nchi mbili, ambaye hana uchungu na nchi yetu kiasi cha kutuchochea tupigane kisha arejee kwao. Ninalosema, gesi itunufaishe sote kama Watanzania. Nimemsikia Zitto ameanza tena uchochezi akidai Kigoma kuna mafuta, ila waelezwe watabaki na nini.
Sitanii, kichwa cha makala haya, kinasema: Waislamu wachinje, sisi tule nguruwe wetu. Nimelazimika kuandika makala haya baada ya kubaini sura ile ile ya upotoshaji katika jamii yetu. Mwanza kumeibuka kundi la watu wanaojiita Wakristo kuliko Waroma.
Kundi hili linashinikiza na kuhamasisha utengano katika jamii. Kundi hili limepeleka malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndekillo, likidai Wakristo waruhusiwe kuchinja. Waziri wa Uhusiano wa Jamii, Stephen Wasira, amefika pale akajaribu kusuluhisha mgogoro huu, inaelekea ameshindwa.
Nikisoma katika mitandao naona wakubwa huko Mwanza wameanzisha hadi bucha zao. Wanachinja wenyewe na kuwauzia Wakristo wenzao. Nimejaribu kufuatilia chimbuko la mgogoro huu. Wanasema Waislamu wanawadharau kwa kula nguruwe.
Eti Waislamu wanataka hata maduka ya nguruwe yaliyopo katika mitaa yao yavunjwe kuepusha kukwaza imani yao. Hapo ndipo ninapopingana na Waislamu sawa na nilivyopingana na Wakristo. Katika utawala wa Awamu ya Pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi, nchi yetu ilipata mgogoro kama huu. Mzee Mwinyi alimaliza tatizo hili kwa busara ya hali ya juu.
Balozi Finland: Misitu inaweza kuiinua Tanzania
Misitu ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wa Watanzania ikiwa itatumiwa vizuri, amesema Balozi wa Finland hapa nchini, Sinikka Antila.
JAMHURI yaisafisha TTCL
Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), imemng’oa katika madaraka Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Said Amir, na kuwasimamisha kazi maofisa wengine watatu waandamizi ili kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ufisadi zinazowakabili.
Mangula kazima moto kwa petroli Bukoba
Kwa karibu miezi sita sasa, siasa za Jimbo la Bukoba mjini zimegeuzwa siasa za chuki, kutishana, fitina, kuchambana, kulaumiana, kuonesha umwambwa, uwezo wa kifedha, dharau, ubaguzi na ujenzi wa matabaka yanayosigana katika jimbo hili.