Author: Jamhuri
FIKRA YA HEKIMA
Wengine waige Vodacom kuwajali wafanyakazi
Kampuni ya Vodacom Tanzania ni mfano mzuri wa kuigwa, katika uwasilishaji wa makato ya fedha za wafanyakazi wake kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Ni ujinga CHADEMA kupinga uzazi wa mpango – (3)
Fikiria maisha ya mijini, vyumba vya kupanga utaishia kulaza watoto wanne katika chumba kimoja, katika kitanda kimoja na ndani ya chandarua kimoja. Lakini pia katika maisha ya vijijini gharama zimepanda hata kama unaishi kwenye nyumba yako.
Umoja wa Tanzania ni propaganda
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alituasa kwamba tufanye juhudi kuziba ufa mkubwa uliojitokeza katika Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, na kuendelea kuainisha nyufa nyingine. Lakini ni kama hatukumsikiliza na kumjali.
Tutaijutia amani tunayoichezea
Kwa muda wa mwezi sasa nchi yetu ipo katika migogoro isiyomithilika. Yamekuwapo matukio yanayotia shaka iwapo sisi wazazi tuna hakika na tunachostahili kuwapatia watoto wetu. Kule Mwanza na Geita yametokea mauaji yaliyotokana na mapigano kati ya Wakristo na Waislamu wakigombea kuchinja wanyama.
Utawala Bora hutokana na maadili mema (3)
Hata hivyo, siku hizi umeletwa utaratibu wa kuwa na “semina elekezi” kwa viongozi wote wakuu wa Serikali. Utaratibu huu unatokea mara kwa mara (periodically) pale hitaji la kuwaelekeza wanaohusika na utawala dhima na wajibu wao kitaifa.
Kasi yetu ya kuchimba dhahabu inatisha, idhibitiwe
Mikataba ya kuchimba dhahabu hapa nchini ilianza kusainiwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Mzee Benjamin William Mkapa.