Author: Jamhuri
Mradi wa WB hatarini
*Ni kisima cha maji kilichogharimu Sh mil 50
*Tajiri anataka apewe Sh mil 22 kukinusuru
Wakati Watanzania wengi wakikosa maji safi na salama, mradi wa kisima cha maji eneo la Mpeta katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, uliofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB), uko hatarini kutoweka.
Mbowe afichua njama za CCM
*Asema Sh bil. 29 ni za kuibakiza madarakani
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema Sh bilioni 29 zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya Presidential Delivery Unit (Kitengo cha Kufuatilia Ufanisi wa Miradi), zitatumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha kinabaki madarakani.
Maskini Bunge letu!
Watanzania tumepata mshituko. Tumeshangazwa na mwenendo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumeshangazwa na jinsi siasa zilivyoanza kugeuzwa uadui. Tumeshangazwa na jinsi wabunge walivyoanza kupoteza heshima na kushindwa kujitambua.
Mawaziri wagongana
*Dili ya uwekezaji yawafanya washitakiane kwa Waziri Mkuu
*Wajipanga kumkabili Kagasheki, naibu achekea kwenye shavu
Mawaziri wawili na wabunge kadhaa wameungana dhidi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kukoleza mgogoro ulioibuka Loliondo.
NUKUU ZA WIKI
Nyerere: Napenda vyama viwili vya kijamaa “Mimi binafsi nitafurahi sana kuona Tanzania nayo ikiwa na vyama viwili vya kijamaa; na ikakataa kabisa kabisa kuweka vyombo vyake vya ulinzi na usalama mikononi mwa wapiganaji wa siasa hiyo.” Baba wa Taifa…
TFF, Simba, Yanga wanaua uwekezaji soka la vijana
Karibu kila mdau wa michezo ninayezungumza naye kuhusu mustakabali wa maendeleo ya tasnia hiyo hapa Tanzania, anagusa uwekezaji kwa vijana. Nilivutwa na kuamini katika uwekezaji wa soka la vijana, baada ya serikali kumwajiri kocha wa timu ya Taifa, kutoka Brazil, Marcio Maximo.