Author: Jamhuri
NUKUU ZA WIKI
Nyerere: Chama hakitakiwi kufanya kazi za Serikali “Katika aina yoyote ya utawala wa kidemokrasia, Chama kinachoshika Serikali, hakitakiwi kufanya kazi za Serikali, na haifai kifanye vitendo kana kwamba ndicho Serikali.” Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius…
Wanaofilisi PSPF wajulikana
*Mwenyekiti CCM atajwa, Serikali Kuu ndiyo inaongoza
*Takukuru, Usalama wa Taifa, wafanyabiashara wamo
SERIKALI na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa nchini, ndiyo wanaoelekea kuufilisi Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF). Mfuko unawadai Sh trilioni 6.4. Wafuatao ndiyo wadaiwa wakuu.
RC Arusha anaendekeza ujinga dhidi ya Lema
Miaka miwili iliyopita Rais Jakaya Kikwete alipofanya uteuzi wa wakuu wa mikoa, nilifurahi. Nilifurahi baada ya kusikia wamo vijana walioteuliwa, na hasa mmoja tuliyekuwa tukifanya kazi wote chumba cha habari Majira, Fatma Mwassa. Huyu sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora na anaendelea vyema.
Mchezo wa vinyoya unaweza kuibeba Tanzania Olympics
Hatimaye wadau wamejitolea kuufufua mchezo wa vinyoya, uliopoteza hadhi yake licha ya kuitangaza Tanzania kimataifa miaka ya 1960 na 1970.
Wazungu wamshitaki Waziri Kagasheki
*Yaliyoandikwa na JAMHURI yametimia
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ameshitakiwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Mlalamikaji ni Kampuni ya raia wa kigeni inayojihusisha na uwindaji wa kitalii ya Foa Adventure Safaries Limited.
Yah: Laiti lingepigwa baragumu wafu wafufuke
Kuna wakati huwa naona kama ndoto ninapowakumbuka baadhi ya watu. Namkumbuka sana marehemu baba yangu, kwa mtazamo wake na uamuzi wa kifamilia kwa wakati ule. Naona jinsi alivyokuwa na mtazamo wa kitaifa zaidi na si kifamilia.