Author: Jamhuri
Mengi aanzisha shindano kukabili umaskini Tanzania
. Watu wanatuma mawazo bunifu kupitia Tweeter
. Washindi wazawadiwa Sh mil 1.8 kila mwezi
Katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa umaskini Tanzania, Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi, ameanzisha shindano la mawazo mapya yanayotaja mbinu bora za kutokomeza tatizo hilo.
Tanganyika inarejea, TAKUKURU iko wapi?
Wiki iliyopita Tume ya Marekebisho ya Katiba ilitangaza rasimu ya kwanza. Rasimu hii ina kila sababu ya kusifiwa. Nilipata fursa ya kuwakilisha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kuchambua na kuwasilisha mapendekezo ya tasnia ya habari nchini. Kwa ufupi nasema, asanteni wajumbe wa Tume kwa kusikiliza kilio cha Wanahabari.
Maisha ya mjasiriamali baada ya kustaafu
Wiki iliyopita nilifika katika mmoja ya mifuko ya pesheni kujiandikisha kwa ajili ya utaratibu wa kujiwekea akiba kwa mpango wa kuchangia kwa hiari. Baada ya kutoka katika ofisi za mfuko huo wa pesheni nikiwa na fomu na makabrasha mengi, nikakutana na mtu mmoja ambaye maongezi kati yangu na yeye ndiyo yaliyonisukuma kuandika makala haya.
Wanasiasa mmewasaidiaje wakulima wa pamba?
Msimu wa zao la pamba unakaribia kuanza, huku hali ya ubora na uzalishaji wake hapa Tanzania ukiwa hauridhishi. Kilimo cha Mkataba bado hakijafanya kazi.
Mwalimu Nyerere na mgombea binafsi
Mei mosi, 1995 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa mgeni rasmi kwenye Sherehe za Mei Mosi mjini Mbeya, alizungumza mambo mengi yaliyolihusu Taifa. Miongoni mwa mambo hayo ni haki ya kuwapo mgombea binafsi. Ifuatayo ni sehemu ya maneno hayo ya Mwalimu ambayo sasa yamewekwa kwenye Rasimu ya Katiba Mpya ya mwaka 2013.
NUKUU ZA WIKI
Mwalimu Nyerere: Wanadamu huongozwa na sheria
“Nchi zote duniani huongozwa na wanadamu na si malaika. Wanadamu hawa huongozwa na sheria na si kwa akili zao wenyewe.”
Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius K. nyerere.