Author: Jamhuri
Tandala wakubwa waibeba Ruaha
Hakika kuamini ni kuona. Sikupata kuamini uwepo wa tandala wakubwa hapa Tanzania hadi siku nilipozuru Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na kujionea aina hiyo ya wanyamapori.
Rais + Makamu wawili = Kudumisha Muungano
Mpendwa msomaji, ni katika hali isiyo ya kawaida leo nimelazimika kuandika makala mbili katika Safu hii ya Sitanii. Nimechukua hatua hii kutokana na uzito wa hoja hizi mbili. Mwanzo niliwaza kuzichanganya, lakini nikaona kila moja ina uzito wa ina yake.
CHADEMA, CCM wana siri ya Arusha, Kibanda, Dk. Ulimboka
Mpendwa msomaji, leo najadili mada ya mwelekeo wa kisiasa katika nchi yetu. Nimeijadili mada hii kwa kina katika Kipindi cha ‘Jicho la Habari’ kinachorushwa na Star TV kila Jumamosi asubuhi kati ya saa 1:30 na saa 3:00 asubuhi. Katika mjadala ule, nilijaribu kuangalia mustakabali wa taifa hili.
BONIFACE WAMBURA:
Kiwango cha soka kinakua Tanzania
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeeleza kuridhishwa na ukuaji wa kiwango cha mpira wa miguu hapa nchini. Msimamo huo umetolewa na Ofisa Uhusiano wa TFF, Boniface Wambura katika mahojiano maalum na JAMHURI jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Unaweza kuzalisha fedha za kutosha
Wiki iliyopita niliandika makala yenye kichwa “Imani yako inaakisi fedha zako.” Kama ilivyo ada nimepokea mirejesho mingi kwa barua pepe, simu za miito na ujumbe mfupi. Wasomaji wamekuwa na mitazamo tofauti – wengine wakinipongeza na wengine wakionesha dukuduku.
Rais Obama: Haijapata kutokea
*Manowari, ndege vita kufunika anga la Tanzania
*Mashushushu zaidi ya 60 kumlinda akiwa D’Salaam
*Vioo maalumu visivyopenya risasi vyaletwa toka USA
Rais Obama anayetarajiwa kuwasili hapa nchini wiki ijayo, ziara yake itakuwa na mambo mengi ya kusisimua na kuonesha ukwasi wa Taifa hilo lenye nguvu za kijeshi na kiuchumi kuliko taifa lolote katika sayari hii ya dunia.