JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Hongera Kikwete, Membe; Salva rekebisha kasoro hii

 

Julai 1 na 2 zilikuwa siku za pekee katika historia ya Tanzania. Tanzania ilihitimisha kilele cha ugeni mkubwa kuja hapa nchini ndani ya mwaka mmoja. Katika siku hizi taifa lilikuwa na ugeni mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Obama.

 

Afrika inaelekea kutawala uchumi Afrika (1)

 

Nawasalimu wasomaji wote, ninawapongeza na kuwashukuru wote ambao wamekuwa wakiwasiliana nami. Mbarikiwe. Itakumbukwa kuwa huko nyuma nimepata kuandika makala iliyokuwa na kichwa, ‘Naiona Afrika ikiinuka tena’.

 

Obama ampandisha chati Lowassa

Hatua ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion Ubungo jijini Dar es Salaam, imeamsha mjadala mzito katika jamii uliowafanya Watanzania kuanza kumhurumia Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wakiona alionewa.

Tulichojifunza kutoka ziara ya Obama

Rais Barack Obama wa Marekani aliingia Tanzania Jumatatu Julai 1, mwaka huu, akaondoka Jumanne Julai 2. Mambo mengi yalitokea wakati wa ziara yake. Mengine ni mazuri tuyaendeleze, mengine ni mabaya tujisahihishe. Yote hayo ni mafunzo tuliyopata kutoka ziara ya rais huyu wa Marekani mwenye asili ya Afrika.

NUKUU ZA WIKI

Julius Nyerere: Mahitaji ya wananchi yalindwe

“Lazima tuendelee kuhakikisha kwamba mahitaji ya msingi ya watu wote yanapatikana na yanalindwa. Lengo letu lazima liendelee kuwa kuinua hali ya maisha ya kila mtu, na kila mtu aweze kupata huduma za msingi za elimu na matibabu.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mkutano Mkuu Simba kuamua hatima ya Rage

Mkutano Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club ya Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika Julai 15, mwaka huu, jijini ndiyo utakaoamua iwapo Mwenyekiti wa timu hiyo, Ismael Aden Rage, ataendelea kushika wadhifa huo au la.