Author: Jamhuri
Katiba mpya iakisi uzalendo (1)
*Uraia wa nchi mbili haufai, tuuache
Baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoa Rasimu ya Katiba mpya kwa wananchi kuitafakari, nchi nzima imelipuka. Natumia neno kulipuka kusisitiza furaha ya wananchi kwa tukio hili.
Barua ya wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
Mheshimiwa Rais Jakaya M. Kikwete, kwa unyenyekevu na heshima ninaleta ombi la kuonana nawe ana kwa ana nikueleze shida inayonikabili.
FASIHI FASAHA
Ombaomba ni unyonge wa Mwafrika
“Unyonge wetu ni wa aina mbili, unyonge wa kwanza ulio mkubwa zaidi ni unyonge wa moyo; unyonge wa roho. Unyonge wa pili ndiyo huu wa umaskini wa kukosa chochote. Ni kweli hatuna chochote, hatuna nguvu.” Haya ni maneno ya Mwalimu Nyerere alipowahutubia walimu katika Sherehe za Vijana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Mei 30, 1969.
Nchi imetafunwa!
*Hazina yatumia Shilingi bilioni 8, taasisi za umma
zachangishwa, ‘wajanja’ watafuna mamilioni
*Vifaa vya Obama vyaokoa jahazi, sare, mikoba, vyagharimu
mil. 400/-, vinyago navyo balaa!
*Karamu, chupa za kahawa, miavuli mil. 390/-,
Burudani ya muziki yatafuna milioni 195/-
*Dewji agoma kuchangia, Katibu Mkuu Haule
arushiwa kombora, yeye ajitetea
Mkutano wa Majadiliano ya Kimataifa ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue), uliomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, umeigharimu Serikali Sh bilioni nane.
Sakata la Iddi Simba bado bichi
*Ikulu, ofisi ya CAG washangazwa kuachiwa
*Uamuzi uliofanywa na DPP wazua maswali
Kuachiwa kwa mwanasiasa Iddi Simba, ambaye hivi karibuni alikuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kabla ya Mkurugenzi wa Mshitaka nchini (DPP), kuamuru awe huru, kumeibua mgongano mkubwa serikalini.
Waraka kutoka mtandaoni
Wanaosoma Ujerumani wamlilia Kikwete
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, kwanza naomba niombe msamaha kwa kutumia forum hii badala ya kukuandikia binafsi. Hii ni kwa sababu ya dharura ya jambo lenyewe linalohitaji hakika hatua za haraka sana ili kuokoa haya yanayotokea. Hivyo, naomba unisamehe kwa kuweka bayana hili hapa.