Author: Jamhuri
Hofu yatanda uwekezaji Kurasini
. Wanaohamishwa hawajui watakacholipwa
. RC Dar, diwani wawataka wavute subira
. Tibaijuka, Nagu watafutwa bila mafanikio
Hofu ya kuchakachuliwa fidia imetanda miongoni mwa wananchi wanaohamishwa kupisha ujenzi wa Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa katika Kata ya Kurasini, jijini Dar es Salaam.
Mradi huo utajengwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China katika eneo lenye ukubwa wa hekta 670 (sawa na ekari 1,675). Inaelezwa kuwa kiasi cha Sh bilioni 90.4 kimetengwa kugharimia ujenzi huo.
NUKUU ZA WIKI
Julius nyerere: Usipowapa wengi watanyakua
“Utaratibu wowote unaowanyima wengi haki yao hauwezi ukaitwa demokrasia… Waswahili wanasema: Wengi wape, usipowapa watanyakua wenyewe.”
Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakati akihimiza demokrasia ya kweli.
Muhudumu Muhimbili aeleza vibweka vya mochari
Ni kawaida kwa vijana kuomba kazi katika ofisi za mashirika na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali zenye mazingira mazuri kiutendaji, lakini imekuwa tofauti kwa vijana hao kuomba kazi katika Chumba cha Kuhifadhia Maiti (mochari). Hatua hiyo…
Matusi kwa Rais wetu hayakubaliki
Kwa muda sasa, kumekuwapo maneno mengi kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda yakimlenga Rais wetu, Jakaya Kikwete. Chanzo cha yote haya ni mapendekezo ya Rais Kikwete ya kumwomba Rais Kagame aketi na waasi wa kundi la FNBL ili kukomesha mapigano na mauaji yanayoendelea Rwanda na upande wa mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Obama amedhihirisha ugaidi ni tishio
Tanzania imepata bahati ya kutembelewa na Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye ni miongoni mwa viongozi wakuu maarufu wachache duniani. Marekani ni taifa lenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi. Ni miongoni mwa mataifa yanayounda Umoja wa G8 – yaani mataifa manane yenye nguvu za kiuchumi na kijeshi duniani.
Utajiri wa Loliondo na laana yake (3)
Sehemu iliyopita, mwandishi alieleza namna watu wa koo za Boroko la Loita kutoka Kenya walivyoingia Loliondo na kuonekana ndiyo wakazi halali wa eneo hilo. Anaeleza pia chanzo cha mgogoro Loliondo akisema ni vita ya uchumi ambayo sasa imepata kasi kutokana na raia wa kigeni na NGOs zinazofadhiliwa na mataifa ya Ulaya na Marekani. Endelea.