Author: Jamhuri
Pikipiki zinatumaliza, DPP futa aibu hii
Kwa muda sasa yamekuwapo maelezo ya kuonesha jinsi pikipiki zilivyo janga la kitaifa. Pikipiki zimekuwa zikishutumiwa kwa kusababisha ajali, kupoteza nguvu kazi na kuongeza idadi ya walemavu au vifo kwa kasi ya ajabu hapa nchini.
Ukitaka mafanikio halisi lipa kodi kwa uaminifu
Kwa hivi sasa mashine za kielektroniki za EFD za TRA, imekuwa ndiyo habari ya ‘mjini’ kwa wafanyabiashara karibu kila kona nchini. Hii imekuja baada ya awamu nyingine ya TRA kujumuisha wafanyabiashara wengi zaidi tofauti na ilivyokuwa mwanzo wakati zikiingia.
Siri za Ponda kupigwa risasi zavuja
Siri nzito zimevuja juu ya sababu za Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kupigwa risasi mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Wakati Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, akiliambia gazeti la Daily Telegraph la Uingereza Jumamosi usiku kuwa polisi ndio waliompiga risasi Ponda wakati anajaribu kukimbia, magazeti ya Tanzania Shilogile ameyaambia hajui kilichotokea.
Kweli Tanzania si shamba la bibi?
Toleo lililopita kupitia gazeti hili nilitoa makala yenye ushauri kwa Rais Jakaya Kikwete asizungumzie usalama wa nchi nyingine na ajikite kutatua matatizo ya kiusalama na tishio la kutoweka kwa amani kwenye nchi yetu kabla ya kuwashauri viongozi wa nchi nyingine.
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Tusiruhusu wachache kuishi kifahari
“Kama watu wachache wanaishi maisha ya fahari fahari, na watu walio wengi hawapati hata mahitaji yao ya lazima, hatutaweza kudumisha amani na utulivu nchini mwetu. Ni muhimu sana kwa chama chetu na serikali yake kulizingatia jambo hili kwa makini.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Murray atolewa kombe la Rogers
Bingwa wa Wimbledon katika mchezo wa tenisi, Andy Murray ameshindwa katika mashindano ya mchezo huo baada ya kufungwa mpinzani wake Ernests Gulbis katika raundi ya tatu ya kombe la Rogers Cup mjini Montreal.