Author: Jamhuri
Wajasiriamali na mfupa wa huduma kwa wateja
Siku moja nilikuwa mjini Mafinga wilayani Mufindi katika Mkoa wa Iringa. Nikiwa hapo niliingia kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi nikiwa na lengo la kununua vifaa kadhaa vyenye thamani ya takribani shilingi laki tatu.
Ray C awalaani wauza ‘unga’
Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, amewalaani watu wanaofanya biashara ya kuuza dawa za kulevya nchini, akisema wanaharibu maisha ya vijana wengi.
Ponda naye anatafuta huruma ya waumini?
Mtakumbuka kuwa Agosti 10, mwaka huu, siku ya Idd Pili, iliisha vibaya kwa Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda. Siku hiyo katika simu yangu uliingia ujumbe mmoja kutoka kwa watu zaidi 25. Ujumbe huo ulisomeka hivi ‘Sheikh Issa
Ponda amepigwa risasi Morogoro, wataarifu waumini wengine kumuombea na kukemea mashambulizi ya silaha dhidi yake’.
Mtendaji mkuu Osha alalamikiwa Tughe
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, amelalamikiwa mbele ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), kuwa anawaongoza kimabavu wafanyakazi wa taasisi hiyo ya Serikali.
Madudu ya mgodi wa Geita yaanikwa
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unadaiwa kukwepa kulipa kodi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kiasi cha Sh bilioni 38.2 tangu mwaka 2007 hadi 2013.
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Tujifunze kusikiliza hoja za wengine
“Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zilizotolewa na wenzetu, na kuzijibu kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama aliyezitoa ni rafiki au si rafiki.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.