Author: Jamhuri
TPSF: Tunataka sera ya kuwapendelea wazawa
Huenda Watanzania wataanza kunufaika ipasavyo na rasilimali za nchi, ikiwa Bunge litaridhia hoja ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) inayotaka ianzishwe sera ya upendeleo maalum kwa wazawa katika ugawaji zabuni na maeneo ya uwekezaji.
Bashar al-Assad: Mbabe anayeitikisa Dunia
Kwa zaidi ya miezi kumi nchi ya Syria imeingia katika mzozo uliosababisha machafuko makubwa nchini humo na kusababisha watu zaidi ya 1300 kupoteza maisha. Mzozo huo unasababishwa na wananchi wa nchi hiyo kutoikubali serikali inayongozwa na Rais Bashar al-Assad.
KAULI ZA WASOMAJI
Daraja la Mbutu vipi?
Pongezi kwenu waandishi wa Gazeti JAMHURI kwa kutujulisha habari zenye weledi. Kero yangu ni ujenzi wa daraja la Mbutu. Kasi ya ujenzi wa daraja hili umekuwa wa kusuasua, na masika karibu yanaanza. Jamani mnaohusika na ujenzi huu fanyeni haraka kuukamilisha
Ngara walitabiri Rwanda kuisambaratisha EAC
Wahenga walisema asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Kwa Bukoba nilikotokea wanasema ‘akagunjua kalafa tikaulila nzamba’ (ka-mnyama ka-kufa huwa hakasikii baragumu). Baragumu ni njia ya mawasiliano iliyokuwa ikitumiwa tangu enzi. Hata wauza samaki kwa Bukoba huwa wanatumia baragumu (olukuri) wanapotembeza (wanapouza) samaki.
Je, kufanya biashara ni kipaji?
Msomaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Jackson, alinitumia pongezi na kuniuliza swali hili: “Sanga, kwanini wataalamu mnasema biashara ni kipaji? Usemi huu una maana gani? Na mfano hai, tazama jamaa zetu Wahindi, kwa Watanzania angalia Kanda ya Kaskazini – Wachagga; kwa Nyanda za Juu Kusini angalia Wakinga. Unasemaje hapo?”
Katika makala ya leo nitajikita kulijibu swali hili.
Bahati nzuri ni kwamba nimesoma Shahada ya Biashara nikiwa chuo kikuu na huu mjadala wa ikiwa biashara ni kipaji ama la ulikuwa ni sehemu ya ‘assignments’ zetu katika somo la Ujasiriamali (Entrepreneurship). Mjadala huu unapatikana katika kitu wanachokiita tetesi (myths) kuhusu ujasiriamali.
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Kujidai unajua kila kitu ni hatari
“Kiongozi anayejidai kuwa anajua kila kitu, na kumbe hajui, ni hatari zaidi kuliko yule anayekiri kuwa hajui kitu na yuko tayari kujifunza.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Alizaliwa 1922, akafariki 1999.