JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Safari hii ya Goma ihitimishiwe Kigali

Meja Khatibu Mshindo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amekufa katika mapambano nchini DRC. Amekufa kishujaa. Amekufa akitekeleza maelekezo halali ya Umoja wa Mataifa (UN) yanayolenga kuwafanya wananchi wa Mashariki mwa DRC waonje tunu ya amani. Kifo cha kamanda huyu kinapaswa kiwe chachu kwa Watanzania na wapenda amani katika Afrika na duniani kote.

Matakwa ya Rwanda yasiivunje EAC

Kwa muda wa mwezi mmoja sasa uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umezorota. Uhusiano huo umezorota baada ya matukio mawili. Tukio la kwanza ni ushauri  Rais Jakaya Kikwete aliompa Rais Paul Kagame wa kuzungumza na waasi wa kundi la FDLR kwa nia ya kurejesha amani. La pili ni Tanzania kupeleka majeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na waasi wa M23.

Matapeli wakubwa Tanzania hadharani

RIPOTI MAALUM

*Watumia madini kutapeli Wazungu hadi bilioni 160/-, watamba

*Mwanza, Dar, DRC, Zambia, Papa Msofe, Aurora waongoza ‘jeshi’

*BoT, NBC, Exim Bank, Polisi, Mahakama, Uhamiaji nao watumika.

 

Baada ya sifa ya Tanzania kuingia doa kutokana na watu wengi maarufu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa matajiri wengi nchini wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kutupwa kwa Wazungu kupitia ahadi hewa za kuwauzia madini.

Arsenal, Man City kibarua kigumu UEFA

Hali inaonesha kuwa timu za Arsenal na Manchester City huenda zikapata wakati mgumu kufuzu katika michuano ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA) kutokana na muundo wa makundi yanayozijumuisha timu hizo.

Bosi wa Masogange anaswa na ‘Unga’

 

*Anaswa na kilo 50 Nairobi, zinafanana na za wanamuziki

*‘Unga’ wagonganisha majaji, mahakamani watafutana

Wakati Mahakama Kuu ikituhumiwa kuharibu mwenendo wa kesi za dawa za kulevya nchini kwa kutoa hukumu zinazopingana na sheria zilizotungwa na Bunge, mtu anayetuhumiwa kuwa ndiye aliyewapatia mzigo wa kilo 180 za dawa za kulevya wanamuziki, Agnes Jerald (Masogange) na Melisa Edward waliokamatwa Afrika Kusini Julai 5, naye amekamatwa na ‘unga’.

Uhamiaji yamrejesha kwao wakala wa Kaseja

 

Ni yule wa FC Lupopo ya Kongo

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imemrejesha rasmi, Ismail Baduka, ambaye alikuwa wakala wa golikipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ile ya kuishi nchini na kuendesha shughuli zake bila ya kuwa na kibali maalum.