Author: Jamhuri
Historia itaihukumu CCM Oktoba
Ninaanza mada hii kwa kuyanukuu maneno ya Fulton J. Sheen aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki huko Marekani. Alinena; “Usiogope kukosolewa kama upo sahihi, na usikatae kukosolewa kama hupo sahihi.” Kwa sababu ninakwenda kuzungumzia mustakabali wa Taifa letu, inanilazimu kukosoa…
Kaaya abisha hodi Arumeru
Elirehema Moses Kaaya ni mwanasiasa asiyekata tamaa. Ni kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) anayeamini katika falsafa, itikadi, katiba na imani ya chama hicho japo anakerwa mno na masuala yanavyokwenda ndani ya chama hicho tawala na kikongwe nchini. Amegombea ubunge…
Wa kuiokoa CCM ni Lowassa
Utafiti nilioufanya kwa takribani miaka miwili kuanzia Aprili 2013 hadi sasa juu ya hali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), nimebaini mambo mengi, lakini kwa makala ya leo nitagusia tu aina ya kiongozi atakayefaa kukiongoza baada muhula wa Rais Jakaya Kikwete…
Huu sasa ni mparaganyiko
Ningali nakumbuka siku niliposikia neno hili “MPARAGANYIKO”. Mara ya kwanza, sikulielewa. Ilikuwa mwaka 1979 kama mwezi Aprili hivi, nikiwa nafanya kazi Visiwani Zanzibar katika vikosi vya SMZ. Niliwajibika kuwamo katika misafara ya ziara za Rais visiwani. Siku ya siku, kulikuwa…
Serikali makini haiwezi kusarenda
Nilipomuona Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudence Kabaka, akitengua uamuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) wa kuwataka madereva kurejea darasani, nilishangaa. Nilikuwa miongoni mwa tuliopigwa na bumbuwazi kwa uamuzi huo, ingawa walikuwapo mamia kwa maelfu…
Yah: Bidhaa feki na soko huru la Tanzania bila kipingamizi
Tangu nilipozaliwa hadi leo, sijapata kujiridhisha kama kweli naweza kula kitu ambacho kimetengenezwa kwa kemikali na mbwembwe nyingine, lakini kikawa na afya na virutubisho vya kweli katika mwili wangu. Sijawahi kufikiria kuwa naweza nikapata huduma mbalimbali kwa njia ya mkato…