Author: Jamhuri
Maalim ajivua lawama Z’bar
Sasa ni dhahiri. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ametabiri hatari ya mgawanyiko unaoweza kuikumba Zanzibar, lakini asingependa alaumiwe kwa uamuzi utakaochukuliwa Zanzibar. Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Serikali ya Mapinduzi wametangaza…
Ufisadi mwingine Uhamiaji
Ikiwa zimepita wiki mbili tangu Rais Dk. John Magufuli awasimamishe kazi Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, na Kamishna wa Fedha na Utawala, Piniel Mgonja, mambo mapya yameanza kuibuka. Vyanzo vya habari kutoka ndani ya idara hiyo vinasema Serikali imefanya…
Kinyesi, damu kero Kimara
Wakazi wa Mtaa wa Kimara Stopover, Dar es Salaam wamelalamikia kero ya kinyesi na damu ambavyo vimekuwa vikisambaa katika makazi yao kutoka machinjio ya Suka. Wakazi hao wameieleza JAMHURI kwamba kutokana na kukithiri kwa uchafu huo, afya zao zimekuwa hatarini…
Ofisa KCMC atuhumiwa kuajiri Warundi
Ofisa Utumishi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Kilimanjaro, inayomilikiwa na Shirika la Msamaria Mwema (GSF), Alpha Chabakanga (57), anatuhumiwa kuwaajiri raia wanne wa Burundi katika shughuli za ujenzi wa nyumba yake. Pia anatuhumiwa kuvunja haki za binadamu kwa kumtumikisha…
Maalim Seif na uchu wa madaraka
Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amedhihirisha wazi kuwa yeye ni kiongozi mwenye tamaa ya madaraka iliyopitiliza, tamaa inayomwezesha kuteketeza hata nchi nzima pamoja na wananchi wake ilimradi yeye abaki kuwa kiongozi mkuu. Kilichofanya asiweze…
TEF yapata safu mpya ya uongozi
Mhariri Mtendaji wa Gazeti JAMHURI, Deodatus Balile, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Balile alichaguliwa katika nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mjini Morogoro. Katika uchaguzi huo uliojaa ushindani, Balile alipata kura 47 na kumshinda…