Author: Jamhuri
Hekaheka uchaguzi TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linakwenda kufanya uchaguzi wake, huku aliyekuwa Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, akiwa miongoni mwa wagombea ambao mpaka wikiendi walikuwa wamechukua fomu za kugombea tena nafasi ya uongozi. Malinzi amekuwa Rais wa TFF,…
JWTZ waingia Rufiji
Kikosi maalumu cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kimepelekwa katika wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, kukabiliana na genge la majahili linaloendesha mauaji ya askari, viongozi na wananchi wasio na hatia. Kikosi hicho kinatajwa kuundwa…
Sijasikia ACCACIA wakijitetea, namsikia Mtanzania Tundu Lissu akiwatetea!
Sijasikia ACACIA wakijitetea, bali namsikia Mtanzania mwenzetu Tundu Lissu katika maandishi na video zinazoenezwa mtandaoni kwa kasi ya ajabu akiwatetea kwa nguvu na kwa pumzi zake zote. Ni kuhusu mchanga wenye madini uliozuiwa na Serikali bandarini. Amezungumzia mambo ambayo nitayajibu…
IPTL ‘bye bye’
Kuna kila dalili kampuni ya kufua umeme ya IPTL kutopata leseni ya miezi 55, kama ilivyoomba, kutokana na maombi hayo kuja wakati wananchi wakiwa bado na hasira na kampuni ambayo ilihusika na uchotwaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti maarufu…
Ni wakati sahihi kuachana na wanyonyaji
Katika mambo ambayo yamekuwa kero kwa Watanzania kwa kipindi kirefu, ni pamoja na suala la mikataba ya siri ya uchimbaji madini, mikataba ya ufuaji umeme baina ya mashirika na Shirika la Umeme nchini (TANESCO). Suala la usiri katika mikataba ya…
Wananchi Kigamboni wasotea umeme
Wakazi wa Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam, wameulalamikia uongozi wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa kushindwa kusambaza umeme kwa wateja wapya, licha ya kulipia huduma hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Wakizungumza na JAMHURI kwa nyakati…