JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

MAISHA NI MTIHANI (20)

Kujikosoa ni mtihani, unapowanyoshea wengine kidole, vitatu vinakuelekea wewe na  kidole gumba kinasema Mungu ni shahidi. Kwa msingi huu kujikosoa ni mtihani. “Si namna tunavyofanya makosa kunakotutambulisha bali namna tunavyoyasahihisha,” alisema Rachel Wolchin. Kuna kitendawili kisemacho: “Kipo lakini hukioni.” Jibu ni…

Siasa zisiwagawe mama zetu

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yalifikia kilele wiki iliyopita. Shamrashamra zilikuwa nyingi karibu maeneo yote ndani na nje ya nchi. Wanaotambua na kuthamini utu wa mwanamke, kwao hadhi ya mwanamke iko palepale muda wote. Hawasubiri siku maalumu kulitambua au kulionyesha…

AINA TATU ZA SWALI Elekevu, jinga na pumbavu 

Mimi naamini mazungumzo yoyote kati ya mtu na mtu (au watu) yana maana na madhumuni yake. Yanapata uimara na thamani ya maana yanapojengewa maswali yenye nguvu ya hoja na kupata majibu yaliyosheheni ukweli na usahihi. Mazungumzo, maswali na majibu hayana budi…

Yah: Kwanini viongozi wengi hawakufanana na Ruge?

Naandika waraka huu nikiwa najua fika kwamba kuna majonzi juu ya majonzi kwa watu wengi, hasa tasnia ya habari hapa nchi. Wengi wamesikia misiba na ambao hawajasikia ni vema wakajua sasa hata kwa kuuliza. Naandika waraka huu nikiwa na maswali…

P-Square wana utajiri wa kutisha

Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya duniani, hasa Afrika, kundi la P-Square si geni masikioni mwao kutokana na kazi zake kukubalika katika makundi mbalimbali. Vijana hao wawili, ambao ni mapacha kutoka nchini Nigeria, Peter Okoye na Paul Okoye, wanaunda kundi…

Hesabu kali zapigwa Kombe la FA

Asikwambie mtu, hakuna timu isiyopenda kuitwa timu ya kimataifa, miaka ya hivi karibuni msemaji wa zamani wa Yanga, Jerry Muro, alikuwa akijigamba kuwa timu hiyo ni ya kimataifa kwa sababu wanapanda ndege na wanashindana na timu za nje ya Tanzania….