JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Jenerali Waitara awatumia salamu majangili

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Jenerali mstaafu George Waitara, amewatumia salamu wanasiasa na viongozi wa Serikali ambao, kwa namna moja ama nyingine, wamekuwa nyuma ya wahalifu wanaojihusisha na ujangili. Waitara amewataka wote wanaojihusisha na ujangili…

Tusibishanie zika

Wiki iliyopita, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti taarifa ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kuhusu kuwapo kwa ugonjwa wa zika hapa nchini.  Taarifa hiyo ya utafiti wa NIMR, ilitolewa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu…

Dozi ya Waziri Mkuu kwa NGOs za Loliondo

Kwa miaka mingi, eneo la Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, limekuwa kama ‘jamhuri’ ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Eneo hili lenye utajiri mkubwa wa wanyamapori, limekuwa likiongozwa na asasi zisizo za serikali (NGOs) zenye nguvu za…

Ndugu Rais utapimwa kwa uwezo wako wa kuleta mabadiliko!

Ndugu Rais, katika Uchaguzi Mkuu uliopita Watanzania katika ujumla wao walitaka mabadiliko. Kwa kushupalia mabadiliko, mgombea Edward Ngoyayi Lowassa aling’ara kuliko wagombea wenzake wote! Washabiki wake wengi walimtaka kwa sababu tu aliongea lugha waliyoitaka kuisikia, ya kuwaletea mabadiliko! Imani ya…

Vita ya wakulima, wafugaji ni janga

Nianze makala kwa kumshukuru Mungu ambaye kwa huruma yake anatujaalia afya njema katika maisha yetu ya kila siku. Tangu tupate Uhuru Desemba 9, 1961 hadi sasa, nchi yetu imekuwa na sifa kubwa ya Watanzania kuishi kwa utulivu na amani.   Kusema…

Adha ya ‘Double allocation’ (2)

Ndipo akateuliwa Jaji Mihayo kuisikiliza. Huyu naye alianza kuisikiliza upya. Kesi imenguruma kwa Jaji Mihayo kuanzia tarehe 01/12/2006, ikaendelea tarehe 13/04/2007, 26/06/2007, 10/07/2007, 02/11/2007. Kutokana na maombi ya wavamizi kwa Jaji Mihayo barua Kumb. Na. Mushy/A58/LND ya tarehe 03 Julai…