JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Takriban watu 34 wameuawa shambulizi la Israel kaskazini mwa Gaza

Mashambulizi ya anga ya Israel kwenye jengo la ghorofa tano la makazi huko Beit Lahia kaskazini mwa Gaza yamesababisha vifo vya takriban watu 34, shirika la ulinzi wa raia la eneo hilo linasema. Shirika hilo, lililonukuliwa na AFP, lilisema wengi…

Waziri Chana akutana na balozi wa Italia nchini

Na Happiness Shayo – Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Giuseppe Sean Coppola ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kushirikiana kwenye…

Tunduru wauza korosho zenye thamani ya bilioni 62.159/-

Na Mwandishi Maalum,Tunduru KILO milioni 19,375,896.00 za korosho zenye thamani ya Sh.bilioni 62,159,126,758.00 zimeuzwa na wakulima wanaohudumiwa na Chama kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma(Tamcu Ltd). Korosho hizo zimeuzwa katika minada minne kupitia mfumo wa stakabidhi ghalani chini ya usimamizi wa mfumo soko la bidhaa(TMX) ulioonyesha mafanikio makubwa kwa wakulima kupata soko la uhakika na bei nzuri ya zao hilo. Meneja Mkuu wa Chama kikuu cha Ushirika wilaya ya Tunduru(Tamcu Ltd) Marcelino Mrope alisema,mnada wa kwanza ulifanyika katika kijiji cha Nakapanya kilo 1,804,369.00 zenye thamani ya Sh.5,792,024,490.00 zimeuzwa kwa bei ya Sh. 3,210 kwa kilo moja. Mrope alisema,katika mnada wa pili uliofanyika katika kijiji cha Mtina  wakulima wameuza  kilo 7,543,517.00  zenyethamani ya Sh.23,973,297,026.00 kwa bei ya Sh. 3,178. Kwa mujibu wa Mrope,mnada wa tatu uliofanyika kijiji cha Airpot kata ya Mbesa, kilo 5,190,191.00 zimeuzwa kwa bei ya Sh.3,212 huku wakulima wakipata zaidi ya Sh. 16,670,893,492.00  na katika mnada wanne uliofanyika tarehe 12 Novemba kijiji cha Ligoma kilo 4,837,819.00 zenye thamani ya Sh.15,722,911,750.00 ziliuzwa kwa bei ya Sh.3,250. Mrope amewataka wakulima wa korosho, kuhakikisha akaunti zao za benki zinakuwa hai ili kuepusha usumbufu wakati wamalipo kwani baadhi ya wakulima wamekuwa wakipata changamoto ya kutopata fedha kwa wakati. Alieleza kuwa,katika mchakato wa mauzo ya korosho hadi sasa hakuna usumbufu wowote na wakulima wanapata fedha zao kwa wakati, na wanunuzi wanafanya malipo kupitia Chama kikuu cha Ushirika tofauti na hapo awali ambapo malipo yalipitia kwenye Amcos. Mrope,amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake  kutaka  malipo ya wakulima yanafanyika kupitia chama kikuu kwani yamerahisisha sana ulipaji fedha za wakulima kutoka siku 14 hadi siku 4 tangu  mnada unapofanyika. “kwa mfano tumefanya mnada leo haizidi hata siku tano tangu mkulima alipouza mazao yake,kwa hiyo tunaona ni maendeleo makubwa sana,lakini tunaomba wasimamizi wetu waendelee kusimamia na kutoa maelekezo pale zinapojitokeza changamoto mbalimbali katika uuzaji na ununuzi wa mazao ya wakulima”alisisitiza Mrope. Kwa upande wake meneja wa bodi ya Korosho Tanzania Tawi la Tunduru Shauri Makiwa alisema,katika msimu wa mwaka huumazao yote yanayouzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani bei yake imekuwa nzuri na kuwapongeza wakulima kwa jitihada wanazofanya mashambani. Amewasisitiza waendelee kutumia pembejeo kwa wakati ili waweze kupata mavuno mengi na bora yatakayokuwa na bei nzuri, badala ya kutumia pembejeo feki zinazochangia kuwarudisha nyuma licha ya juhudi kubwa wanazofanya mashambani. Mokiwa,amewashauri wakulima wa korosho kuepuka kuchuma korosho zikiwa juu ya miti badala yake kusubiri hadi zinapodondoka chini na kuhakikisha wanaanika angalau kwa siku tatu hadi nne kabla ya kufikisha ghalani ili kuepuka kuwa na unyevu. Mkulima wa korosho wa kijiji cha Airpot kata ya Mbesa Ismail Mpepo,amefurahishwa na bei ya korosho mwaka huu kwanihaijawahi kutokea kwa miaka ya hivi karibuni. Ameishukuru Serikali kwa kusimamia vizuri mfumo wa stakabadhi ghalani uliowezesha wakulima kupata soko la uhakika na bei nzuri, hali iliyohamasisha wakulima wengi kufufua mashamba waliyoyatelekeza kwa muda mrefu.

TNBC yazindua kikundi kazi ‘Uchumi wa Buluu’

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam Kikundi kazi cha Baraza la Biashara nchini (TNBC) kwa ajili ya kuangalia fursa za kiuchumi zitakazopatikana kupitia Uchumi wa Buluu kimezinduliwa jijini Dar es Salaam, huku wajumbe wa kikundi hicho kutoka sekta sekta…

Dk Chimbi apongeza mshikamano ulioonyeshwa na Watanzania kuanguka kwa jengo Kariakoo

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amepongeza utayari na mshikamano ulioonyeshwa na Watanzania mara baada ya tukio la kuanguka kwa jengo Kariakoo, akisema kuwa hatua hizo zimeonesha…