Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia Athumani Baseka (39), fundi seremala na mkazi wa kijiji cha Kamhanga wilayani Geita kwa tuhuma za mauaji ya Faida Lucas (34) ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji cha Bugalama.
Tukio hilo lilitokea usiku wa Oktoba 30 majira ya saa sita usiku katika kitongoji cha Mwamushiki kijiji na Mata ya Bugarama Wilaya na Mkoa wa Geita ambapo marehemu alikutwa na mwanamke aliyewahi kuwa mke wa mtu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Safia Jongo amethibitisha na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa kiini cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.