Mwanamke mmoja (50),Mkazi wa Kitongoji cha Mwamboku Kata ya Kashishi Wilaya ya Kipolisi Msalala Mkoani Shinyanga,Sele Luchagula, ameuawa na watu wasiojulikana akiwa anakula kwa kukatwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili hali iliyopelekea kupoteza maisha papo hapo.
Mauaji hayo yametokea Novemba 19 majira ya saa 2 usiku,Katika Wilaya ya Kipolisi Msalala Mkoani humo ambapo marehemu Sele Luchagula alikuwa anakula yeye na watoto wake wawili pamoja na mkamwana wake.
Akieleza juu ya tukio hilo Mtendaji wa Kata ya Mwamboku,Mayenga Tabu,Amesema kuwa amepata taarifa ya tukio hilo ambapo alifika eneo la tukio na kumkuta mwanamama huyo akiwa amepoteza maisha huku akibainisha kuwa tukio hilo ni la kikatili na lakusikitisha sambamba na kutoa wito kwa wakazi wa kata hiyo watoe ushirikiano kwa serikali ili kuwabainisha waliohusika na mauaji hayo.
“Taarifa ya tukio hilo nilizipata majira ya saa 2 na nusu usiku ambapo nilifika eneo husika na kukuta hali halisi ilivyo ambapo Marehemu Sele Luchagula alikuwa amekwisha kupoteza maisha,nawaomba sana wananchi watoe taarifa polisi kwa yule watayekuwa wanamtilia mashaka ili kujua kilichokuwa chanzo cha mauaji hayo”Amesema Tabu.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji hicho,Leornad Mabula,Amesema tukio hilo limewashangaza na kuwastua wananchi wote,licha ya kufanya mauaji hayo hakuna walichokiiba wala kuchukua katika nyumba hiyo.
Nae mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwamboku,Makaranga Lusanika,Ameeleza jinsi tukio lilivyokuwa ambapo watu hao wasiojulikana walifika katika numba hile na kumkuta marehemu Sele akiwa na watoto wake na mwe wake mmoja ambapo waliwaambia wapo chini ya ulinzi ndipo wakatekeleza mauaji.
“Majira ya saa 2 Walifika watu wasiojulikana ambapo wakawakuta wenye nyumba wakiwa wanakula ndipo wakawaambia wakae kimya na wasiende popote,hapo ndipo walipomkata mapanga marehemu Sele hali iliyopelekea kifo chake”Amesema Lusanika.
Aidha baada ya kumtafuta kamanda wa Polisi Mkoa Shinyanga,ACP Janeth Magomi kwaajili ya kutoa uthibitisho wa tukio hilo la mauaji alisema hajapata taarifa zozote za mauaji hayo huku akiomba kupewa muda kwaajili ya kufuatilia zaidi