Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi,Dar es Salaam
Askari wa Jeshi la Polisi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam wametoa msaada wa vifaa Tiba katika Zahanati ya Jeshi la Polisi iliyopo chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kwa lengo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutimiza miaka kumi nane ya utumishi ndani ya Jeshi la Polisi tangu walivyo ajiriwa mwaka 2005.
Akipokea vifaa hivyo leo Agosti 16,2023 Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amewashukuru askari hao ambao wameonyesha mfano wa kuingwa kwa jamii ya askari wa Jeshi hilo kwa kutoa vifaa tiba ambapo amebainisha kuwa vitaasaidia kutatua changamoto ya vifaa tiba katika Zahanati ya chuo hicho.
SACP Dkt. Mambosasa ameongeza kuwa si askari tu wa Jeshi hilo watakaofaidika na vifaa hivyo bali Jamii nzima inayozunguka Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam watakwenda kunufaika na vifaa hivyo.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Jeshi la Polisi ambae ni Mkufunzi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam INSP Lule Mlay amesema wametimiza miaka kumi na nane ambapo wametoa vifaa hivyo ikiwa ni shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda tangu wameajiriwa na Jeshi hilo.
Nae mwanafunzi wa kozi ya uofisa Sarafina Chamlonde ametoa wito kwa askari wengine wanaotimiza miaka kadhaa kazini kutoa msaada kwa wahitaji na makundi mengine katika Jamii.