Na Mwamvua Mwinyi, JAMHURI MEDIA Pwani.
Mkuu wa Operation wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Nassoro Sisiwaya amewaasa madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali za mara kwa mara.
Ameyasema hayo Mkoani Pwani akiwa kwenye operesheni maalumu ya kukamata magari yanayovunja sheria za usalama barabarani nyakati za usiku.
Operesheni hiyo imeweza kukamata makosa 32 ambapo madereva wa magari 22 walikamatwa kwa kosa la mwendokasi, madereva 7 walikamatwa kwa kosa la kuzidisha abiria kati ya magari hayo 7, magari 2 ni mabasi makubwa ya abiria na magari 5 ni coster na magari 3 yalikamatwa kwa kosa la ubovu.
Aidha, zoezi hilo lilifanikiwa kukamata magari 18 yenye taa moja maarufu kama chongo kati ya magari hayo 18 magari 15 yakiwa ni magari ya abiria 13 aina ya coster na maroli 5.
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kinatoa onyo kali kwa madereva wote wanaoendesha vyombo vya moto hususani nyakati za usiku kuto kuingiza magari yao barabarani iwapo yana mapungufu ya aina yoyote.
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani linaendelea na operesheni hii ya kukamata madereva wa magari yanayovunja sheria za usalama barabarani kwa nchi nzima .
Pia linaendelea kuchukua hatua kali ikiwemo kufungia leseni za madereva hao na kuwafikisha Mahakamani kwa watakaotiwa hatiani.