Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Kamos Hamad amewataka askari wa Jeshi la Polisi kuendeleza mazoezi ya karate kwa lengo la kuongeza ukakamavu na kujiamini.

Akipokea vifaa vya michezo kutoka Jumuiya ya Korea Friend of Hope huko Madungu, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba CP. HAMAD amesema ni vyema askari wakatumia fursa ya uwepo wa ukumbi na walimu wa karate kupata mafunzo ya Mchezo wa Karate.

Nae Kim Keumhoon kutoka Jumuiya ya Korea Friend of Hope amelishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano waliowapatia na kuwaruhusu kuendeleza mchezo huo kwa Askari na wananchi wa maeneo jirani.
Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Polisi, Kamisheni ya Zanzibar.

Please follow and like us:
Pin Share