Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Serikali imewahakikisha wananchi wanaofanya shughuli zao kupitia mitandao kuwa wapo salama zaidi na Serikali imetunga Sheria ya kulinda data za mtu binafsi katika matumizi ya mtandao na kila mtumiaji analindwa na hairuhusiwi kutumia data za mtu bila ridhaa yake.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Habari , Mawasiliano naTeknolojia ya Habari Jerry Slaa,alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili linalojadili upatikanaji wa huduma bora za uhakika na kasi za matumizi ya mtandao wa Internet kwenye Ukumbi wa hotel ya Grain Melia Jijini Arusha.

Amesema kwamba matumizi ya mtandao wa Intanenti yamekuwa ni maisha ya kawaida ya Watanzania na sio starehe tena na hivyo ni jambo ambalo kila mtu anapaswa kuwa nayo.

Amesema asilimia 75 ya Watanzania kila mtu ana miliki simu ya mkononi ambapo zaidi ya Wananchi milioni 35 wanatumia huduma ya mtandao wa Internet ikiwemo shughili za kilimo na biasha.

Waziri Slaa,amesema sasa 89 ya Watanzania wanapata huduma mtandao lengo ni Wananchi wote wapate huduma ya mtandao wa Internet,simu ,habari ,redio na televisioni yakuwemo maeneo ya Utalii ambayo yamepewa kipaumbele

Amesema Serikali mwezi May mwaka jana ilizindua ujenzi wa minara 758, kupitia USAF ,na kuna mfuko imeutengeneza ambao kila mtoa huduma anauchangia ili kupeleka huduma kwenye maeneo ambayo wafanyabiashara hawawezi kupeleka kwa sababu hayana tija ya kibiashara kwao.

Amesema kuna minara mingine 636 mradi huo utaanza Oktoba mwaka huu katika kuhakikisha maeneo yote nchini yanapata huduma hiyo.

Amesema kuna mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kuwaunganisha Wananchi kwenye mtandao wa Internet na kufikia miunganiko bora zaidi wenye uhakika ,gharama nafuu,usiokuwa na hitilafu ili kuwe eza kuendelea kuunga mkono shughuli mbalimbali za Kiuchumi na kijami.

Naye Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya simu za mkononi,Airtel ,Joseph Muhere, amesema mwaka jana kampuni hiyo imefunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa na una uwezo mkubwa wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani ambazo zinahitaji mawasiliano kwa njia ya mtandao.

Amesema kuwa kampuni hiyo mwaka huu 2024 inaendelea kufangua huduma zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini kuwezesha kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G.

Muhere, amesema kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo sasa wanajenga huduma ya 5G kwa ajili ya wateja Ujenzi ambao unaenda sambamba na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu.

Mkutano huo umewakutanisha wadau wote wa mawasiliano nchini ikiwemo Airtel Tanzania chini ya kauli mbiu ya ‘Meaningful Connectivity’.

Airtel wataonyesha namna gani Mkongo wa Chini ya Bahari wa Airtel 2 Africa utakavyochangia katika maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha mawasiliano kote nchini pamoja na namna ambavyo mkongo huo utasaidia kuiweka Tanzania kama kinara wa kidigitali katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Eng. Cecil Francis ,amesema Shirika hilo lina dhamana kubwa ya kutoa huduma bora za mawasiliano kupitia mkongo wa taifa ambao ulianza kutekeleza mwaka 2013.

Amesema kuwa TTCL inafanya kazi ya kuhakikisha nchi inaongea kwa kuunganisha mkoa kwa mkoa ,Wilaya kwa Wilaya ambapo tayari wilaya 106 kati ya 139 zimeshaunganishwa kwenye mkongo wa taifa.
Amesema kuwa mkongo huo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano ambao umeunganishwa na mkongo wa bahari ambayo ndio inatupa Internet.

Amesema kuwa wameunda mkongo huo na nchi jirani za Kenya,Uganda ,Rwanda,Burundi ,Zambia,Malawi na kuna maunganusho yanayoenda kwenye mpaka na Msumbijina sasa wanaanza kushughulikia maunganusho na nchi ya DRC Congo,kupitia ziwa Tanganyika hadi mji wa Kalemii Nchini DRC.

Cecil amesema wanashugulikia maunganisho kwenda kwenye kituo kilichopo baharini hadi Mombasa Nchini Kenya.

Amesema TTCL inaendelea kutoa mchango wa mawasiliano kuhakikisha mkongo unaojengwa inakuwa na ubora wa hali ya juu kwa lengo la kufikisha huduma kwa Wananchi na kupunguza gharama.

Amesema nchi yetu ni kounganishi kikuu cha Mawasiliano kwenye ukanda wetu wa nchi za EAC na SADC
Amesema Wilaya 33 zilizobakua ambazo hazijaunganishwa kwenye mkongo wa taifa zitaunganishwa mwaka huu na wakandarasi wanaendelea na kazi hiyo.

Please follow and like us:
Pin Share