Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Katavi

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Mpimbwe Dickson Mwenda (37) kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkazi wa Kibaoni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Makame amesema mtuhumiwa anadaiwa kumbaka mtoto huyo ndani ya gari yake yenye namba za usajili T 927 DMC.

Kamanda Makame ameeleza kuwa tukio hilo la unyanyasaji wa kingono lilifanyika Agosti 13,mwaka huu, majira ya saa moja na nusu jioni huko katika Kijiji cha Kibaoni, kata ya Kibaoni.

Ameongeza kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa baa akipata vinywaji na mtuhumiwa ambapo baada ya muda alimuomba awapeleke watoto wake nyumbani ambao walikuwa wawili yaani mtoto aliyebakwa na mdogo wake.
Alieleza kuwa mtuhumiwa alipofika njiani alisimamisha gari na kumbaka mtoto huyo.

Ameongeza kuwa baada ya tukio hilo taarifa zilipelekwa katika kituo cha Polisi na baadae mtuhumiwa alikamatwame.

Aidha Kamanda Makame ameeleza kuwa mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakama kujibu shtaka lake