Timu ya Arsenal imeshindwa kuutumia vema uwanyja wake wa nyumbani kwenye kombe la EUROPA baada ya kwenda sare ya bao 1-1 na Atletico Madrid ya Hispania, goli la Arsenal lilifungwa na Mshambuliaje wake hatari Alexandre Lacazette kwenye dakika ya 61, huku goli la kusawazisha la A. Madrid lilifungwa Antoine Griezmann kwenye dakika ya 82.
Arsenal itajirahumu yenyewe kwani ilikuwa na nafasi pale A. madrid walipokuwa pungufu baada ya Sime Vrsaljko kupewa kadi nyekundu kwenye dakika 10
Kwa matokeo hayo Arsenal itakuwa imejiweka kwenye sehemu mbaya ya kutinga hatua ya Fainali kwani inatakiwa kwenda kushinda ugenini, ni vigumu kwa A. Madridi lakini tusubiri mpira dakika 90 na chochote kinaweza kutokea.
Matokeo mengine katika mechi za jana ni kwamba Marseille imeifunga Salzburg kwa mabao 2-0, mabao ya mMarseille yalifungwa na Florian Thauvin dakika ya 15 na Clinton Njie dakika ya 63
Arsenal (4-3-3):