Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kikosi chake kilijivuta sana na kunusurika dhidi ya klabu ya Sweden Ostersunds FK, hivyobasi kufuzu katika raundi ya timu 16 bora katika kombe la ligi ya Yuropa. Arsenal ilishinda awamu ya kwanza 3-0, lakini karibia ishangazwe baada ya wageni hao kufunga mabao mawili ndani ya sekunde 70.

Kikosi cha Graham Potter ambacho kimepanda kutoka daraja la nne tangu 2010 kilikuwa kifua mbele katika kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza bao la pili kufuatia bao la kujifunga mwenyewe la Calum Chambers kutokana na shambulio la Hosam Aiesh na bao la Ken Sema.

Lakini Gunners ambao walianzisha kikosi thabiti siku tatu kabla ya kushirki katika fainali ya kombe la Carabao dhidi Manchester City iliimarika baada ya kipindi cha kwanza huku Sead Kolasinac akifunga krosi nzuri iliopigwa na Bellerin katika uwanja wa Emirates.

”Hatukujituma katika kipindi cha kwanza” , alisema Wenger ambaye kikosi chake kilizomewa baada ya kipindi cha kwanza na baada ya mechi kukamilika.

”Nadhani katika kipindi cha pili tuliimarika na tungefunga mabao zaidi. Katika kipindi cha kwanza tulikuwa katika matatizo na hatarini kwa sababu tulijivuta sana , hatukuwa na malengo na tulijipata mashakani kila mara tulipopoteza mpira”.

”Hatukuwa na malengo tulipokuwa na mpira na ndio maana tulijipata katika matatizo.Tulijibu vizuri na ndio maana tukafuzu”.

Arsenal ambayo haijashinda kombe la Uefa ama lile la Yuropa watawajua wapinzani wao siku ya Ijumaa.

Ostersund ni klabu ya pili kushinda mechi ndani ya uwanja wa Emirates katika mechi 28 ambazo The Gunners wamecheza kutoka Machi 2017.

MAGOLI YALIVYOFUNGWA

https://youtu.be/DHdSHKE_HkM