Ligi kuu nchini uingereza jana usiku iliendelea kwa kuzikutanisha Arsenal na Liverpool kwenye uwamja wa Emirates, ambapo kulishuhudia wanaume hao wakitunishiana misuli baada ya kufungana mabao 3 kwa 3.

Liverpool walikuwa wakwanza kuandika bao lililofungwa na Philippe Coutinho kwenye dakika ya 26, kipindi cha kwanza. Mpaka mapunziko Liverpool 1 Arsenal 0, Liverpool iliongeza bao la pili kupitia kwa Mohamed Salah kwenye dakika ya 52, na kuufanya ubao usomeke 2-0.

Dakika chache baada ya Arsenal kufungwa bao la pili, washika bunduki hao walichaluka na Alexis Sanchez katika dakika 53 aliweza kuipatia Arsenal bao 1 na dakika 56 Granit Xhaka aliweza kuisawazishia Arsenal bao la pili, na dakika 58 tena Arsena kupitia Mesut Oezil alifunga 3 na kuufanya ubao usomeke 3-2, Arsenal iliweza kufunga mabao 3 ndani ya dakika 6.

Liverpool iliweza kusawazisha bao la tatu kupitia Roberto Firmino kwenye dakika ya 71 mpaka filimbi ya mwisho ubao umesomeka 3-3.
Kwa matokeo hayo Arsenal imebaki kwenye nafasi ya 5 ikiwa na point 34 huku Liverpol ikiwa kwenye nafasi ya 4 ikiwa na point 35.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezo ifuatayo

Everton VS Chelsea

Brighton & Hove Albion VS Watford

Manchester City VS AFC Bournemouth

Southampton VS Huddersfield Town

Stoke City VS West Bromwich Albion

Swansea City VS Crystal Palace

West Ham United VS Newcastle United

Burnley VS Tottenham Hotspur

Leicester City VS Manchester United