Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mbeya
Daines Paul Mwashambo (30), mkazi wa Kijiji cha Mashese aliyekuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu amefariki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema kuwa marehemu alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya na amefariki dunia Machi 9, mwaka huu saa 10:15 jioni.
Kamanda Kuzaga amesema kuwa marehemu akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese – Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu aina ya ‘Pare Force’ watoto wake wawili na kusababisha vifo vyao na kisha na yeye alikunywa sumu hiyo iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu.
Mtuhumiwa aliendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo lakini Machi 9, 2024 alifariki duniani.
Kamanda Kusaga aliwataja watoto wake wawili waliofariki kwa kunyweshwa sumu ya kuulia magugu na mama yako ni Mario Semen Adamson (4) na mdogo wake wa kike aitwaye Beonis Semen Adamson (2) wote wakazi wa Mashese kwa
Amesema watoto hao walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu na walipoteza maisha wakiwa wanaendelea na matibabu
Amesema kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliosababishwa na kutuhumiwa kwa matukio ya wizi na Serikali ya Kijiji cha Mashese.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa jamii kuwa pindi unapopatwa na tatizo suluhisho lake sio kujichukulia sheria mkononi bali ni kutafuta ushauri au kufuata sheria inavyoelekeza ili kuepuka madhara kwa muhusika na jamii inayokuzunguka.