Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue ametangaza kuwa Serikali itaanza kusimika kamera za ulinzi katika ofisi zote za umma, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha utekelezaji wa sheria na kudhibiti mienendo isiyo na maadili na ya kinyume na sheria.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali, imeelezwa kuwa hatua hiyo inalenga kulinda heshima na uadilifu kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanazingatia maadili ya kazi.
Serikali imeweka wazi kuwa haitavumilia mienendo yoyote inayokiuka maadili ya utumishi wa umma, na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa.
Hatua hiyo imekuja nyuma ya tangazo la serikali ya nchi hiyo, hapo jana lililotolewa na makamu huyo wa Rais kuwa serikali itawafuta kazi watumishi wote wa umma watakaobainika kuwa miongoni mwa wanawake zaidi ya 400 waliorekodiwa wakifanya mapenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha la taifa hilo (ANIF), Baltasar Ebang Engonga (54) katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye ofisi za serikali na nyumbani kwa Ebang.
Ebang ambaye ni baba wa watoto sita, tayari amekamatwa kwa kosa la kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na wanawake zaidi ya 400, miongoni mwao inasemekana kuwa wake za watu wakiwemo, mke wa kaka yake, binamu yake, dada wa rais wa nchi hiyo, mke wa mkuu wa ulinzi wa rais wa nchi hiyo, mke wa mwanasheria mkuu wa nchi hiyo na mtoto wa mkuu wa jeshi la polisi la nchi hiyo.
Wengine walioonekana wakifanya mapenzi na Ebang kwenye video hizo ni mke wa mlinzi wake ‘bodyguard’, mke wa mchungaji wake, wake wa mawaziri kadhaa wa nchi hiyo, mke wa mjomba wake ambaye ni mjamzito, marafiki 15 wa mdogo wake wa kike na wanawake wengine mbalimbali ambapo imeelezwa wote hao walionekana kuridhia video hizo kurekodiwa