Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Aliyewahhi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Bill Tendwa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema marehemu Tendwa amefariki leo Desemba 17, 2024 katika Hospitali yall Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Ameaema marehemu aliwahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuanzia mwaka 2001 hadi 2013.
Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa na familia kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Kibamba Hospitali.
Ratiba na taarifa rasmi za mazishi zitatolewa mara baada ya kukamilika.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi.