Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Morogoro

Mtu mmoja aliyehamika kwa jina la Costa Clemence, 22, mkazi wa kijiji cha Maseyu kata ya Gwata Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro amekutwa amefariki dunia na mwili ukiwa umetelekezwa porini katika kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema hayo katika taarifa yake ya matukio mbalimbali ya mkoa huo.

Mkama amesema kuwa mtu huyo alikutwa amefariki dunia Septemba 15, mwaka huu asubuhi na pembeni yake kukiwa na pikipiki isiokuwa na namba za usajiri ambayo inasadikiwa kuwa ni ya marehemu huyo.

Kamanda wa Polisi mkoa amesema kuwa mwili huo ulikutwa hilo la Gwata ambalo halina makazi ya watu na kwamba mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

“Katika tukio hili tupeni muda tunalifanyia kazi, uchunguzi ukikamilika tutawapa taarifa, hakuna kitu kitakachofichwa” alisema Mkama.

Mwenyekiti wa kijiji cha Gwata , Ally Gobole ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio usiku wa kuamkia Septemba 15 mwaka huu akidai walifika watu wasiojulikana nyumbani kwao marehemu na kumchukua kisha kutokomea kusikojulikana.

Amesema baba wa marehemu alitoka nje na kuona watu hao wakitokomea na kijana wake akaanza kuwakimbiza bila mafanikio na hivyo kutoa taarifa kwa kwake yeye mwenyekiti wa kijiji.

Amedai katika tukio hilo walichukuliwa vijana watatu akiwemo Aziz Kimweru akiwa barabarani ananunua chipsi kisha wakamchukua mwingine aitwaye Malinda maarufu kama Jack wakaondoka nao na kwenda k kuwapiga .

Amedai vijana hao wawili ambao ni Jack na Azizi wapofutiliwa walikutwa wamepigwa na kuumizwa vibaya ambao walitoa taarifa ya kifo cha mwenzao huyo Costa na ndipo mwenyekiti na wananchi walitoka kuanza kumtafuta na hatimaye kumkuta amefariki.

Mwenyekiti huyo ameeleza ya kwamba majeruhi hao wamelqzwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu.