Na Magrethy Katengu-Jamhuri Media
Dar es Salaam

Akiba Commercial Bank Plc imeguswa kuendelea kuunga Mkono jamii kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali katika kituo cha kuelelea Watoto Yatima kilichopo Sinza Dar es salaam.

Amebainisha hayo Machi 28,2025 Dar es salaam Bi Dora Saria, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Bank, wakati akikabidhi msaad kituo cha kulea Watoto cha Chakuwama, ikilenga kuboresha ustawi wa watoto na kuleta tabasamu kwenye nyuso zao.

Bi Dora amesema Msaada huo, ambao umetolewa ni mahitaji muhimu, unaonesha dhamira ya Benki hiyo ya kusaidia watu wenye uhitaji na kujenga matumaini kwa mustakabali mwema alieleza na wana inaamini katika kuunga mkono jamii na kuleta mabadiliko chanya ya kudumu

“Akiba Commercial Bank, tunaamini katika nguvu ya mshikamano kwa kubadili maisha. Msaada huu ni hatua muhimu ya kuhakikisha ustawi wa watoto hawa na kuleta matumaini kwa wenye uhitaji kwa maisha bora yajayo,” amesema Bi. Saria.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa kituo hiko cha Chakuwama Hassan Tabu, ameshukuru sanaa Akiba Commercial Bank kwa ukarimu wao, amesema kuwa msaada huo ni mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watoto hao.

“Tunaishukuru sana Akiba Commercial Bank kwa kusimama nasi katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na Kwaresma kwani kutoa ni Moyo wala si utajiri waendelee hivyo hivyo na Mungu awabariki ” ameshukuru Hassan

Aidha Msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watoto na kuwapatia sababu ya kutabasamu,
Kupitia juhudi hizi, Akiba Commercial Bank Plc inathibitisha tena dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii kwa vitendo, ikilenga kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu kwa jamii inayoihudumia.