Dar es salaam, Desemba 12, 2017: Airtel Tanzania mtandao bora kwa Smartphone yako leo imezindua bando mpya zitakazojulikana kama ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ kwa lengo la kuwapatia wateja wake na watumiaji wote wa intaneti bando kabambe za intaneti.
‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ imezinduliwa leo ambapo, takwimu za hivi karibuni kuhusu ongezeko la watumiaji wa huduma za simu toka kwa Mamlaka ya Mawasialino Tanzania (TCRA) zikionesha ongezeko la kiasi kikubwa cha watumiaji wa huduma hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa asilimia 54 huku pia huduma ya Intaneti ndani ya miaka mitano hiyo ikiwa imeongezeka kwa asilimia 135 zaidi hivyo kutoa msukumo kwa watoa huduma kuendelea kutoa huduma zenye ushindani zaidi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchunda wakati wa hafla ya kuzindua huduma ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti, alisema Airtel tutaendelea kuleta huduma zenye bora na zenye ubunifu wa hali ya juu ili kuendelea kutoa suluhisho kwenye mahitaji ya wateja wetu hasa katika huduma za mtandao wa intaneti ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa Airtel tumejiwekea miakakati mingi kwa kuipa mikakati hiyo kipaumbele zaidi kwa lengo la kukidhi uhitajika na wateja wote”
“Tuaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa suluhisho la mawasiliano kupitia uzinduzi wa ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ kwa kuendelea kutoa huduma nafuu ya Intaneti kwa watumiaji wote nchini huku tukiweka kipaumbele zaidi katika ubora wa mtandao pamoja na kuwapatia wateja uhuru zaidi” aliongeza Nchunda.
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni zawadi ya awali kabisa tunayowapatia watumiaji wa Airtel katika msimu huu wa sikukuu, tunaamini kuwa ndani ya msimu huu wa sikukuu wateja wanauhitaji mkubwa sana wa intaneti katika kukamilisha mawasiliano yao na ndugu, jamaa na marafiki wakati wote, hivyo kuwepo kwa bando hizi za gharama nafuu kuliko zote kunatudhihirisha Airtel kuanza vyema shamrashamra za sikukuu na wateja wetu kwa kuwapatia uhakika wa kutoishiwa bando kwa muda mfupi, ukiwa na SMATIKA hakuna kuzima intaneti tena!”
Akifafanua jinsi ya kujiunga Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano alisema “ Ili kuweza kufaidi bando za SMATIKA na Yatosha Intaneti unatakiwa kupiga *149*99# au pia unaweza kujiunga kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kisha chagua 5 Yatosha Intanet”.
Bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wetu nchi nzima kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kujipatia MB 40 vilevlie ofa kabambe ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu” alieleza Bi Singano
Airtel Tanzania imekuwa katika programu ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano yake ili kukamilisha lengo lake la kutoa mawasiliano bora na yenye uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya U900. Tayari Airtel imezindua maboresho ya mtandao wake kwa kutumia teknolojia hiyo ya U-900 kwenye mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza huku ikiendelea kuwahakikishia wateja wake mawasiliano bora hasa katika maeneo ya nje na ndani ya majengo marefu au yenye uhitaji zaidi.