Na Manka Damian , JamhuriMedia, Mbeya
KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida wananchi wa kata ya Itezi mtaa wa Gombe Kusini Mkoani Mbeya wamelazimika kumfukuza msibani mwanaume mmoja aitwaye ,Seleman Lukama baada ya kumtelekeza kwa miaka 14,mke wake Anna Anosyesye na watoto wake sita.
Inaelezwa kuwa baada ya kupata taarifa za kifo cha mke wake April 26,2025 mwanaume huyo alijitokeza na kufika nyumbani kwake hapo hivyo na wananchi na uongozi wa mtaa Gombe kuamuru . mwanaume huyo aondoke mara moja kijijini hapo kutokana na kitendo alichofanya cha kutelekeza familia yake kipindi cha miaka 14.

Akizungumza na wananchi msibani hapo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Itezi Gervas Mwaseba alisema katika mchakato wa wawahitaji katika katika kata hiyo ilipendekeza marehemu Anna Anosyesye ajengewe nyumba ya kuishi kutokana na mazingira magumu aliyokuwa akiishi na watoto wake .
“Itatupa mkwalizo mkubwa kama wamemdanyanya kuwa mama huyo alikuwa na mume kwa Imani ile ile huyu marehemu hakuwa na mume hivyo tuwaite wathaminishaji wa nyumba na kuandikwa jina mojawapo la mtoto ambaye ndiye atakuwa mrithi wa nyumba na kulea wadogo zake na huyu mwanaume atafute nyumba ya kuishi nyingine,anatushangaza huyu mwanaume mwezetu ukiacha familia wewe ni mwanaume chotara kwa kweli umetudharirisha wanaume wenzio”alisema mwenyekiti huyo.
Hata hivyo Mwaseba alisema kuwa wanaamini kuwa watoto hao ni yatima wanaendelea kuhudumiwa na chama ,na kusema kuwa watasimamia nyumba inayojengwa chini ya Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na mkurugenzi wake ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson mpaka nyumba kukamilika na hati ya nyumba iandikwe watoto.
Janet Kabuje ni Barozi shina namba tisa kata ya Itezi mtaa wa Gombe kusini amesema kuwa mwanaume huyo alimtelekeza mke wake na watoto sita kwa miaka 14, na kwa kilichofanywa na mwanaume huyo sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia za kutekeleza familia zao .
” Mimi mama Claudia nimechota nae maji Kwenye matololi stendi ya Usangu kwa shida kabla hajaanza kuumwa ambapo maji hayo alitumia kufyatua tofari za kujengea nyumba yake ,huyu baba akiwa hayupo na aliondoka na mwanamke wa hapa hapa mtaani kwetu na huko alikokuwa akiishi alikuwa na maisha mazuri tu huko ,lakini ulichofanya kwa familia yako kwa miaka 14 ,ni kitendo cha aibu Sanaa na ni kweli nilikuona pale hospitali lakini kwa ulichofanya hichi ni kitendo cha aibu leo sheria ichukue mkondo wake ili funzo kwa Wanaume wengine wenye tabia kama hizi “amesema Kabuje.

Mwenyekiti serikali ya mtaa wa Gombe Kusini, Amesema ameanza kuumwa hakuwahi kufahamu kama ana mume na kusema kuwa kabla ya kuanza kuumwa marehemu alienda kwa Mwenyekiti kueleza kukimbiwa na mume na kumuacha na watoto sita .
Aidha amesema baada ya kuhojiwa msibani hapo Mume wa marehemu aliomba msamaha mbele ya waombelezaji msibani hapo na kusema alikuwa anakuja na kuondoka na kusema hana la kuongea zaidi ya kuomba msamaha.
Kitendo alichofanya Mwezetu huyu mwanaume ametudharisha Sana kitendo cha kutekeleza mke na watoto ni cha aibu Sanaa hivyo huyu mwanaume aliona ndoa aliyofuata ndo bora zaidi kuliko familia yake ya mke na watoto sita.
Taasisi ya Tulia Trust ilimwibua Marehemu Anna Anosyesye ilifika nyumbani kwa Anna wakati wa kukimbiza mbio za bendera za upendo katika kata ya Itezi mtaa wa Gombe kusini.